Kampuni ya PUMA Energy imeandaa futari maalum Zanzibar, ikikusanya pamoja wateja wake, viongozi wa dini na serikali , na wadau wakuu kwa jioni ya shukrani, mshikamano, na tafakari katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Puma
Energy Bi. Fatma Abdallah amesema lengo la futari hiyo ni kuimarisha umoja
kwani ushirikiano walionao umesaidia sana kufanikisha biashara zao hapa
Zanzibar.
Aidha, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
ina matarajio makubwa ya kutanua huduma muhimu zitakazowafikia wananchi kupitia
miradi ya uwekezaji inayoanzishwa hapo nchini.
Akizungumza katika hafla hiyo,
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Seif Abdallah Juma
amesema lengo la kuwepo miradi hiyo ni kukuza sekta ya huduma na biashara ili
kukuza pato la nchi
Kampuni ya Puma Energy Tanzania ni wauzaji wa aina mbali mbali za mafuta ya vyombo vya moto na vilainishi; Imekuwepo Zanzibar tangu mwaka 1994 (wakati huo ikijulikana kama BP Tanzania)

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar Ndg.Seif Abdallah Juma akijumuika na Wafanyakazi na wageni waalikwa katika hafla ya Iftaar ya pamoja iliyoandaliwa na Kampinu ya Pima Energy Tanzania iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanza wa Ndege Zanzibar.
No comments:
Post a Comment