WAUMINI wa Dini ya Kiislamu Zanzibar wakiwa katika viwanja vya Masjid
Jamiu Zinjibar Mazizini Jijini Zanzibar,
wakifuatilia hatuba ya Sala ya Eid Al Fitry, iliyofanyika leo 31-3-2025, baada
ya kumalizika kwa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Viongozi wa
Serikali,Viongozi wa Dini na Wananchi, wakifuatilia hutuba ya Sala ya Eid Al
Fitry, ikisomwa na Sheikh Khamis Gharib Khamis, baada ya kumalizika kwa Sala ya
Eid iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Jijini Zanzibar
iliyofanyika leo 31-3-2025 na (Kushoto kwa Rais) Mifti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh.Saleh Omar Kaab na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Othman Ngwali na
(kulia kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria, Utumishi na
Utawala Bora Zanzibar Alhajj Dkt. Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa
Rais wa Zanzibar Alhajj Othman Masoud Othman. 





RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Waumini wa Dini ya
Kiislamu katika kuitikia dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Hassan
Othman Ngwali, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Fitry, iliyofanyika
katika Masjid Jamiu Zinjibar leo 31-3-2025 baada ya kumalizika kwa Mwezi
Mtukifu wa Ramadhani, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh
Omar Kaab na (kulia kwa Rais) Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Alhajj Dkt.
Haroun Ali Suleiman na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhajj Othman
Masoud Othman
BAADHI ya Viongozi wa Dini wakijumuika katika
kuitikia dua ikisomwa na Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali,
baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Fitry, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Jijini
Zanzibar leo 31-3-2025

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mufti Mkuu wa Zanzibar
Sheikh. Saleh Omar Kaab, baada ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Fitry
iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Jijini Zanzibar leo
31-3-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman
anayefanyia Kazi zake Zanzibar Mhe. Said Salim Al Sinawi , baada ya kumalizika
kwa Sala ya Eid Al Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini
Jijini Zanzibar leo 31-3-2025.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana Mtoto Samir Idrissa, baada
ya kumalizika kwa Sala ya Eid Al Fitry iliyofanyika katika Masjid Jamiu
Zinjibar Mazizini Jijini Zanzibar leo 31-3-2025
No comments:
Post a Comment