Habari za Punde

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARYAM MWINYI AZINDUA WIKI YA AFYA ZANZIBAR(ZANZIBAR AFYA WEEK 2025)ZANZIBAR.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi  akikata Utepe kuashiria Uzinduzi wa Programu ya Shehia Afya 2025,Afya Bora Maisha Bora katika hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Afya Zanzibar (Zanzibar Afya Week 2025)iliofanyika katika Viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi  akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali akionesha Bango la Ufunguo kuashiria Uzinduzi wa Programu ya Shehia Afya 2025,Afya Bora Maisha Bora katika hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Afya Zanzibar (Zanzibar Afya Week 2025)iliofanyika katika Viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar.


Na Rahma Khamis Maelezo
      8/5/2025

Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi amesema kuwa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation imejidhatiti kuhakikisha kwamba wananchi wa Zanzibar wanapata huduma za  afya zilizobora na zenye kiwango.

 

Ameyasema hayo wakati akizindua Wiki ya Afya Zanzibar katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Wilaya ya Magharibi “B” amesema wiki hiyo ni muhimu kwa kuhamasisha jamii juu ya upatikanaji wa huduma bora za Afya.            

 

Amesema kuwa wiki hiyo pia ni fursa adhimu kwa jamii kwani itawawezesha kuchunguza na kufahamu afya zao pamoja na kupatiwa huduma stahiki.

 

Akizungumzia kuhusu vifo vya mama na mtoto mama Mariam amesema kuwa vifo vimepungua kwa asilimia kubwa kutokana na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kupunguza matatizo katika afya ya uzazi.

 

Wakati huo huo Mama Mariam amezindua programu tatu za kuimarisha afya ikiwemo Afya ya mama na mtoto 2025, Lishe Bora 2025 pamoja na Shehia afya programu 2025.

 

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassoor Ahmed Mazuri amesema kuwa wiki hiyo ina lengo la kuimarisha na kuhamasisha jamii juu ya masuala ya afya na huduma bora.

 

Amesema kuwa maradhi yaziyoambumiza yamekuwa yakiongezeka kwa kasi hivyo wiki hiyo inawapa fursa wananchi mbalimbali kuchunguza afya zao na kupatiwa matibabu. 

 

Aidha amefahamisha kuwa wiki hiyo inaongeza mashirikiano katika utoaji wa huduma zenye kiwango kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali. 

 

Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Mngereza Mzee Miraji amesema kuwa katika kuboresha afya za wananchi Serikali inaendelea kufatilia na kusimamia huduma ya mama na mtoto kwa kupanga Mipango mbalimbali ya dira ya taifa 2050

 

Ameeleza kuwa jumla ya watumishi wa umma 500 wamepatiwa mafunzo na kuwaomba viongozi na wafanya kazi wa afya kuendelea kushirikiana katika sekta hiyo.

 

Wiki ya afya Zanzibar imeanza Mei 4 na inatarajiwa kumalizika Mei 10 ambapo katika wiki hiyo wananchi 1264 wapima afya zao na kupatiwa huduma ndani ya siku tatu.













No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.