Alhajj Hemed ameyasema hayo katika chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Taasisi ya Pondeza Foundation Hafla iliyifanyika katika viwanja vya Hotel ya Maruhubi Beach Villa Maruhubi Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameeleza kufurahishwa kwake na Uongozi wa Pondeza Foundation ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza wa kuendeleza kawasaida na kujumuika na watoto yatima katika Chakula cha Mchana Kipindi hiki cha Eid na kuwataka viongozi na wenye uwezo kuiga mfano huo ili Mayatima nao wafarijike katika siku hii tukufu.
Amesema Dini ya kiislamu imeeleza umuhimu wa kuwahurumia Mayatima na Faida zake ikiwemo kuwa karibu na Mtume Muhammad (S.A.W) katika Pepo ya darja ya juu.
Aidha ameahidi kutoa Kila aina ya ushirikiano katika kuendeleza jambo hilo ili liwe endelevu siku hadi siku kwa Maslahi ya sasa na hata baada ya kufa.
Nae Mwenyekiti wa Pondeza Foundation Mheshimiwa Ussi Salum Pondeza ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Chumbuni amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kujumuika na watoto hao hatua ambayo inaonesha kuunga Mkono juhudi hizo na kuwa karibu nao hasa katika siku za Eid.
Amesema Pondeza Foundation imekuwa na kawaida ya Kuandaa Hafla hiyo Kila ifikapo Eid Adh'ha ili kutafuta Radhi za Allah Mtukufu pamoja na kufurahika na watoto hao.
Akitoa Salamu za Ofisi ya Mufti Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Khalid Ali Mfaume amesema Uislamu umehimiza kwa wenye uwezo kuwalea Mayatima ili wapate Malezi mema ya kumjua Mola wao.
Zaidi ya watoto yatima mia Tano na hamsini (550) wamejumuika katika Hafla hiyo ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Taasisi ya Pondeza Foundation kwa lengo la kuwapatia furaha katika siku tukufu ya Eid.
No comments:
Post a Comment