Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango
akifanya mazungumzo na Viongozi
wa shirikisho la Makampuni
ya Italia (FEDERISPARMIO) yaliyofanyika
Jijini Roma nchini Italia tarehe 23 Juni 2025.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa shirikisho la Makampuni ya Italia (FEDERISPARMIO) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Guido Mucelli, Mazungumzo yaliyofanyika Jijini Roma nchini Italia leo tarehe 23 Juni 2025.
Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa ubia baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni mbalimbali zilizo chini ya shirikisho hilo kufanya uwekezaji kwenye sekta mbalimbali za kimkakati.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa shirikisho la Makampuni ya Italia (FEDERISPARMIO) mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Jijini Roma nchini Italia leo tarehe 23 Juni 2025. (wengine ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Cosato Chumi pamoja, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme Kaimu Mkuu wa Kituo cha Ubalozi Italia, Eva Kaluwa pamoja na Mkurugenzi Msidizi Idara ya Uwekezaji Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Fadhil Chilumba.
No comments:
Post a Comment