Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.
Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.
Baadhi ya vijana wakipewa mafunzo ya utimamamu wa mwili kwa ajili ya kulinda na kuzuia mtoto usiharibu miti ya mashamba ya miti Sao Hill.
Zoezi hilo limefanyika leo Juni 16, 2025 katika viwanja vya Shamba la Miti Sao Hill likishirikisha wahifadhi wa Shamba, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi, likilenga kupata vikosi vitakavyohudumu katika Makao Makuu ya Shamba pamoja na Tarafa ya II ya Shamba Ihefu.
Akizungumza katika zoezi hilo Mhifadhi Mwandamizi anayesimamia Utumishi na Utawala Felista Bayo amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 Shamba linatarajia kuajiri watumishi wa muda 192 kwa ajili ya kukabiliana na kupambana na majanga ya moto kwa kipindi chote cha kiangazi.
Ameongeza kuwa licha ya maombi kuwa mengi kulinganisha na nafasi zilizotajwa, Shamba la Miti Sao aaHill lina shughuli nyingine zinazoendelea katika vituo vyake vyote ikiwa ni pamoja shughuli za bustani na usafi wa mashamba, hivyo wanaokosa nafasi katika vikosi hivyo wanapata fursa ya kuendelea na shuguli nyingine za Shamba.
Kwa upande wake Mhifadhi anayesimamia Kitengo cha Ulinzi wa Msitu dhidi ya moto Murya Sawa amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hili ni matarajio ya TFS kupitia Shamba la Miti SaoHill kuwa watumshi hawa muda waliopata nafasi watafanya kazi hiyo kwa weledi kwa kutanguliza uzalendo huku akihimiza ushirikiano baina ya wananchi wote wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi katika kulinda rasilimali za misitu.
Naye Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Mufindi Ashery Kitundu amesema kuwa lengo mama la jeshi la zimamoto ni kuhakikisha matukio ya moto hayatokei kwa kutoa elimu, na kuyadhibiti pindi yanapotokea hivyo ni watumishi hawa wa muda watakuwa mabalozi wazuri katika maeneo yao waliyotoka kwa kushirikiana na jeshi la zimamoto katika kutoa elimu ya kuepuka na kukabilina na majanga ya moto.
Usaihili huo unatarijiwa kuendelea hapo kesho katika Tarafa ya Kwanza ya Shamba Irundi kisha Tarafa ya Tatu Ihalimba, na Tarafa ya Nne Mgololo.
No comments:
Post a Comment