Habari za Punde

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Alhajj Kassim Majaliwa Ashiriki Sala ya Eid El-Adhaa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Viongozi wa Bakwata na Serikali, wakati alipowasili katika Viwanja vya Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025, ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza la Eid El Adhaa Kitaifa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akijumuika na waislamu katika Sala na Baraza la Eid El Adhaa iliyofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025. ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifuatilia mawaidha baada ya Sala na Baraza la Eid El Adhaa iliyofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025, ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza hilo.
Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Khamis Ngeruko, akizungumza baada ya Sala na Baraza la Eid El Adhaa lililofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025, ambapo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikua mgeni rasmi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia kwenye Sala na Baraza la Eid El Adhaa lililofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025. ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza hilo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mjumbe wa Baraza Kuu la Ulamaa, Sheikh Hassan Chizenga, baada ya Sala na Baraza la Eid El Adhaa lililofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025. Katikati yao ni Kaimu Mufti wa Tanzania, Sheikh Ali Khamis Ngeruko.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi wa Morocco nchini, Mhe. Zakaria El Koumiri, baada ya Sala na Baraza la Eid El Adhaa lililofanyika Kitaifa kwenye Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025. ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza hilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia waumini wa kiislamu, baada ya Sala na Baraza la Eid El Adhaa lililofanyika Kitaifa kwenye Viwanja vya Msikiti wa Mohammed VI, Kinondoni jijini Dar es Salaam Juni 7. 2025. ambapo alikuwa mgeni rasmi kwenye Sala na Baraza hilo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita inawaamini na inathamini mchango wa viongozi wa dini wa madhehebu yote.

 

Amesema serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano kati yake na viongozi hao ili kujenga amani, mshikamano na ustawi wa jamii ya watanzania.

 

"Tunaamini mtaendeleza jukumu la kuwasihi watanzania waone umuhimu wa kila mmoja kuwa sehemu ya mchango wa kulifanya taifa hili kuwa tulivu na kuimarisha mshikamano miongoni mwetu."

 

Ameyasema hayo leo (Jumamosi  Juni 7, 2025) alipokuwa mgeni rasmi katika Sala na Baraza la Eid Al Adha iliyofanyika katika Msikiti wa Mohamed VI Kinondoni, Dar es Salaam.

 

Amesema viongozi wa dini wanayo nafasi kubwa ya kuwajenga waumini wao kuwa na staha, ustaarabu, uvumilivu na kutambua kuwa wao ni miongoni mwa wanajamii na kushiriki katika shughuli za kimaendeleo.

 

"Kwa upande wa serikali tunaendelea kujenga misingi ya mshikamano kati ya waumini wa dhehebu moja na dhehebu jingine, tukiwa tunaamini kuwa dini zimeendelea kuifanya nchi hii kuwa nchi ya amani wakati wote." 

 

Kadhalika ametoa wito kwa watanzania kuendelea kulinda amani na utulivu uliopo nchini ili nchi iendelee kupata ustawi.

 

Amesema ni vyema kuwa na uwezo wa kukemea vitendo vyovyote ambavyo vinaashiria kutishia amani nchini.

 

Aidha, amewasihi watanzania kuendelea kuwaombea viongozi wa kitaifa hususan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ili Mungu ampe nguvu na afya ya kuendelea kuliongoza taifa hili.

 

Kadhalika, amewapongeza waislamu waliofanikiwa kutimiza ibada ya Hijja huku akitoa wito kwa waislamu waliopo nchini kuendelea kuwaombea warudi salama.

 

"Tuendelee kuwaombea wenzetu wakamirishe ibada hiyo, kwetu sisi ni baraka kwa sababu hata sisi wanatuombea."

 

Pia amewapongeza viongozi wa dini kuendelea kutoa mafunzo kwa vijana wadogo ili wakue kwa kuzingatia misingi imara ya kuendeleza dini na maadili yake.

 

"Dini zina ujenzi mkubwa kwa muumini kiimani na tunapowajenga waumini wetu kiimani tuwaingizie imani yenye manufaa kwa taifa".

 

Naye, Kaimu Mufti wa Tanzania Sheikh Ali Khamis Ngeruko, ametoa wito kwa watanzania kuwa makini wakati wa uchaguzi ili wachague viongozi wenye weledi kwa kumpima namna anavyo wasilisha sera zake.

 

"Dunia imekuwa na changamoto kubwa ya watu wenye afya ya akili hivyo tunapo wachagua viongozi tuwachague watu ambao afya zao za akili ziko kwenye kiwango cha juu na kinachoridhisha."

 

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Alhaj Nuru Mruma, amesema Baraza hilo linawahimiza watanzania kuendelea kuilinda amani iliyopo nchini ili kutoa nafasi kwa shughuli za kimaendeleo kufanyika.

 

"Baraza linatoa wito kwa kila Mtanzania kwa nafasi yake kulinda na kudumisha amani, kwani bila amani hakutakuwa na maendeleo yoyote katika jamii".

 

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,                      

JUMAMOSI, JUNI 07, 2025


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.