Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla Amekabidhiwa Fedha Kwa Ajili ya Kumchagia Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Mwinyi

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amefurahishwa na vijana wa chama cha madereva na mafundi  wa serikali pamoja na waendesha boda boda wa Mkoa wa Kusini Pemba  kwa kuendelea kumuunga mkono Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Akizungumza na vijana hao waliofika ofisini kwake Vuga kwa lengo la kumkabidhi fedha taslimu kwa ajili ya kumchangia Rais Dkt Mwinyi katika kuchukua fomu ya kugombea urais wa Zanbiar.

Amesema ni vyema vijana wa Zanzibar kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Hussein Mwinyi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea chaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Amewataka vijana waendeleea kuhubiri na kukumbushana umuhimu wa kuitunza  Amani na mshikamano uliopo nchini.

Aidha, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesisistiza kuwa  Amani ndio msingi wa maendeleo yaliyopo nchini, hivyo amewaasa vijana hao  kutokubali kutumika vibaya kwa maslahi ya watu wachache wasiopendelea mema Zanzibar.

Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Siasa, Itikadi na Uwenezi na mafunzo ya chama cha Mapinduzi komred Khamis Mbeto  khamis amesema vijana wa zanzibar  wamehamasika na kuridhishwa na kazi kubwa iyofanywa na Rais Dkt Hussein Mwinyi ya kuwaletea wananchi wa Zanzibar maendeleo .

Komred Mbeto amemshukuru Makamu wa Pili wa Rais wazanzibar kwa  kusaidia na kumshauri vyema Mhe. Rais katika suala la  malendeleo nchini.

Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya waendesha bajaji na  boda boda Wilaya ya Kusini Pemba Ndugu Seif Said Msellem ameshukuru Mhe. Rais Kwa kutimiza ahadi zake alizoziahidi wakati wa kampeni ikiwa ni pamoja na kurasimisha usafiri wa boda boda kuwa ni biashara rasmi.

Ameahidi kuwa vijana wa Mkoa wa Kusini Pemba watashukana na kuwa mstari wa mbele katika kuilinda Amani iliyopo nchini  hasa kipindi hiki cha kuelekeauchaguzi mkuu.


Imetolewa na kitengo cha Habari (OMPR )
Tarehe 27.08.2025

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.