WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kushirikina na Taasisi ya The Same Qualities Foundation ya Arusha katika kuimarisha Afya za wananchi wa Zanzibar ikiwemo kuwafanyia matibabu watu wenye midomo wazi na kuwa na muenekano mzuri.
Akizungumza mara
baada ya kufanya ziara maalumu katika kambi ya matibabu ya midomo wazi
inayoendelea kufanyika katika Hospitali ya mkoa Lumumba inayoendeshwa na
wataalamu kutoka Taasisi ya The same
qualities Foundation ya Arusha na wataalamu wa hapa nchini Waziri wa Afya
Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amewataka
wazazi wenye watoto walio na tatizo la midomo wazi kufika katika kambi maalumu ili
kupatiwa matibabu.
Amefahamisha
kuwa matibabu yanayotolewa katika kambi hiyo ni bure na dawa zipo za kutosha na kusisitiza kuwa wazazi washirikiane kuwatoa watoto wenye
matatizo hayo majumbani na kuwa peleka
kwenye matibabu, ili kuwapatia furaha na heshima katika jamii watapofanyiwa matibabu ya midomo yao.
Aidha
amesema katika kuimarisha huduma hizo, Taasisi
hiyo imeleta madaktari bingwa wa kutibu matatizo hayo waliotoka nchi mbali mbali kwa lengo la
kuunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Afya Zanzibar ambapo kila mwaka mara mbili Unguja na Pemba wanatoa huduma
hiyo.
Amesema katika
kambi hiyo matibabu hayo yatakwenda vizuri kutokana
kuwepo kwa wengine waliokwenda na matatizo ya kinywa tu na kufanyiwa matibabu
vizuri na wapo vizuri kiafya, wenye matatizo ya midomo wazi walipata matibabu
na wamepona na kuwa na afya nzuri.
Taasi ya The Same Qualities Foundation inafanya
kazi kubwa ya kusaidia jamii kwa kutoa huduma mbali mbali za Afya Tanzania Bara
na Zanzibar hasa kuwapatia huduma watoto na watu wazima wenye midomo wazi na
matatizo ya kinywa kambi hio imeanza matibabu
yake tangu Jumatatu Agust 25 hadi Ijumaa Agust 29 na wanatarajia kuwafanyia
matibabu watu wapatao 25.
mwisho
No comments:
Post a Comment