Habari za Punde

Wizara ya Afya itaendelea kuimarisha huduma za Afya ya msingi kwa wananchi wa Unguja na Pemba

Na.Mwandishi Wizara ya Afya Zanzibar.

WIZARA ya Afya Zanzibar imesema itaendelea kuimarisha huduma za Afya ya msingi kwa wananchi wa Unguja na Pemba hasa huduma za mama na mtoto ili kuondokana na vifo vitokanavyo na uzazi.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Mngereza Mzee Miraji alipofanya ziara katika kituo cha Afya Uzi N'gambwa yenye lengo la kukiwezesha kituo hicho kutoa huduma za kujifungua kwa masaa 24, pamoja na kusikiliza changamoto za kituo hicho.

Amesema Kwa muda mrefu Huduma hiyo ilikua ni tatizo katika kisiwa hicho kutokana na jiografia yake, hali iliyowalazimu kufuata huduma hizo katika kituo cha afya Unguja Ukuu.

Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya imeshapeleka vifaa vitakavyosaidia kuimarisha huduma za Mama na Mtoto katika kituo hicho pamoja na kuwaagiza DHMT Kuhakikisha wanasimamia huduma hizo zinapatikana.

Ameongeza kuwa Wizara ya Afya itahakikisha wafanyakazi wanaohitajika katika kituo hicho wanapatikana wakiwemo wakunga na wauguzi pamoja na madaktari Bingwa wa huduma za mama na mtoto ili kuona huduma hizo zinatolewa kwa ufanisi.

Daktari dhamana wa Wilaya kati Amina Hussein Pandu amesema kutokana na juhudi zilizowekwa na serikali katika kuimarisha huduma bado kituo kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo wafanyakazi na maeneo ya kuhifadhi mazalia.

Aidha amesema kumalizika kwa matatizo hayo ni fursa kubwa ya kuimarisha huduma za za Afya katika kituo hicho pamoja na kutoa wito kwa viongozi kkuangalia uwezekano wa kupeleka madaktari wazawa katika kituoa hicho ili kupata wepesi na urahisi wa utoaji wa huduma hizo.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.