Habari za Punde

Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na washirika wa maendeleo mbali mbali wakiwemo King Salman humanitarian aid and relief Centre

 Na.Mwandishi Wizara ya Afya Zanzibar.

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya itaendelea kushirikina na washirika wa maendeleo mbali mbali wakiwemo King Salman humanitarian aid and relief Centre pamoja na Muslim World League katika kuimarisha Afya za wananchi.

Akizungumza katika kambi ya upasuaji kwa ujumla watoto inayoendelea kufanyika Hospitali ya Kivunge Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano wa Afya Kimataifa Wizara ya Afya Zanzibar Dkt.Juma Ali Makame amesema juhudi kubwa zinafanyika kuhakikisha kuwa zinapelekwa huduma zilizobora kwa jamii kwa karibu.

Amefahamisha kuwa huduma upasuaji wa jumla zinazotolewa katika kambi hiyo ni za kibingwa na lengo kubwa ni kuwasaidia watoto ambao wanamatatizo mbali mbali yanayohitaji upasuaji na kuwataka wananchi wenye mataizo kufika hospitalini hapo kwa ajili ya uchunguzi na kufanyiwa matibabu.

Dkt.Juma  amesema katika kuimarisha huduma za Afya hapa nchini   zaidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imefanya jitihada kubwa ya kuweka miundombinu ya Afya pamoja na madaktari bingwa na bingwa bobezi, vifaa tiba, ili huduma hizo zipatikane kwa urahisi katika Hospitali za Wilaya.

Kwa upande wake Daktari Dhamana wa Hospitali ya Kivunge Haji Machano Haji amesema kambi inayoendelea kufanyika katika Hospitali ya Kivunge si kwanza ni muendelezo wa kuwapatia matibabu wagonjwa mbali mbali katika Hospitali hiyo ambapo kwa awamu hii wamewapatia matibabu ya upasuaji watoto waliochini ya umri wa miaka 12.

Aidha amesema kuwa tangu kuanza kwa kambi hiyo tayari zaidi ya watoto 50 wameshafanyiwa matibabu ya upasuaji na kusaidia faraja kubwa kwa wagonjwa la kuondokana na gharama za matibabu sambamba na madaktari wazawa kupata nafasi kubwa ya kujifunza utaalamu kupitia kwa madaktari kutoka nchini Saudia.

Ameishukuru Serikali ya awamu ya nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kujali afya za wazanzibari kwa kuimarisha miundombinu ya afya pamoja na huduma pamoja na madaktari wazawa kupata ujuzi kutoka nchi mbali mbali duniani.

Hassan Ahmed Katungunya Mkurugenzi wa Taasisi ya Muslim Wold League iliyopo Tanzania Bara amesema kambi hiyo imelenga kuwafanyia upasuaji watoto zaidi ya mia moja na wamekuja na vifaa vya kutosha kufanyia matibabu hayo na kuwataka wananchi wawafikishe watoto kupata matibabu.

Kwa upande wake Daktari mbobezi wa upasuaji kwa watoto Dkt Baiya Abdalla Rashid amesema madaktari kutoka nchini Saudarabia kwa kushirikiana na wataalamu wazawa wameweza kufanikisha utoaji wa huduma ya upasuaji hasa maradhi ya kuzaliwa yanayohusina na utumbo ambapo wapo watoto ambao tangu wamezaliwa haja zao kubwa zinasumbua.

Aidha amefahamisha mara nyingi maradhi ya kuzaliwa mtoto anakosa hisia ya kwenda haja  na tatizo hilo ni la uchango mkubwa unakosa hisia ya kupata choo na mtoto husababisha kupata matatizo ya chango kupandiana ambapo kupitia kambi hiyo watoto wengi wameweza kufanyiwa upasuaji wenye matatizo hayo.

Dkt Baiya amewataka wazee kutokaa na watoto majumbani na watakapoona mtoto hasa wa miezi mitatu anatatizo si la kawaida likiwemo la kukosa haja kumfikisha Hospitalini mara moja kupata matibabu ili kuondokana na matatizo hayo.

Mwisho

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.