Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba akisalimiana na Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma , Mchungaji Stanley Tabulu alipowasili kwenye Usharika wa KKKT Kisasa jijini Dodoma , kushiriki ibada ya Jumapili , Novemba 16.2025. Kulia ni mkewe Mama Neema Mwigulu Nchemba, kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Daniel Sllo na wa tatu kulia ni Askofu wa KKKT Dayosisi ya Dodoma, Askofu Christian Ndosa.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na mkewe Mama Neema Mwigulu Nchemba wakishiriki katika Ibada ya Jumapili kwenye Usharika wa KKKT Kisasa jijini Dodoma, Novemba 16, 2025. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Daniel Sillo.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na Mkewe Neema Mwigulu Nchemba (wa tatu kulia) pamoja na viongozi wengine wakiombewa waliposhiriki katika Ibada ya Jumapili kwenye Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kisasa Dodoma, Novemba 16, 2025. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Daniel Siro.
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akizungumza katika Ibada ya Jumpili aliyoshiriki katika Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kisasa jijini Dodoma, Novemba 16, 2025..JPG)
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba akimsikiliza mkewe Mama Neema Mwigulu Nchemba aliposalimia katika Ibada ya Jumapili aliyoshiriki katika Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Kisasa jijini Dodoma, Novemba 16, 2025.
Baadhi ya washiriki wa Ibada ya Jumapili katika Usharika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Kisasa jijini Dodoma wakimsikiliza Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba alipozungumza katika ibada hiyo aliyoshiriki, Novemba 16, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


No comments:
Post a Comment