Habari za Punde

KASORO NDOGO AFRIKA MASHARIKI ZIPEWE NGUVU- MUSOKYA


Na Yunus Sose, STZ - Gazeti la Zanzibar leo

MAKAMU wa Rais wa Kenya Stevin Kalonza Musokya amesema hakuna haja kwa nchi za Afrika Mashariki kuzipa nguvu kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza zikasababisha vita au kuvuruga azma ya kuanzishwa Jumuia ya Afrika Mashariki.

Alisema nchi za Afrika Mashariki zina histaoria nzuri, hivyo si vyema haistoria hiyo ikavurugwa kwa sasoro ndogo ndogo ambazo zinawezeza kurekebishwa kwa najia za aina kwa ana au kwa diplomasia.

Mosokya aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko hoteli ya Lagema Nungwi Mkaoa wa Kaskazini Unguja.

Amezitaka nchi za Afrika Mashiriki kujipanga upya kuangalia njia zitakazowezesha wazo la kuwepo Jumuia hiyo ambayo kuwepo kwake kuataweza kuongeza naguvu za maendeleo ya uchumi kwa nchi hizo pamoja na wananchi wake.

`Matagizo kama haya ya kisiwa cha Migingo kinacholeta mzozo baina ya Uganda na Kenya si jambo la kufikiria kuanzisha vita baina ya nchi zetu, lakini ni suala la kumalizwa kidiplomasia` alisema Musokya.

Alifahamisha kuwa katika nchi za Afrika Mashariki Tanzania na Kenya zinahitaji kuimarisha umoja na mashirikiano zaidi kwani nguvu za nchi ndizo zitakazoweza kutoa msukumo kwa nchi za Afrika kuanzisha kile ambacho watakifiria kuanziswa katika ukanda huo.

Akizungumzia juu ya ziara yake nchini Tanzania, Musokya alisifu juhudi kubwa zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania na ile ya Mapianduzi ya Zanzibar katika kukuza na kuendeleza sekta ya Utali hali ambayo inaashsiria nchi kupiga hatua kubwa zaidi katika michache ijayo.

Alisema katika ziara yake ameweza kijifunza mengi katika sekta ya Utalii hasa visiwani Zanzibar ambavyo kiwango cha utalii kimeshafikia hali ya juu kabisa.
`
`Naamini kuwa kuna Wakenya wengi na baadhi ya Watanzania mambo kama haya hawayaelewi hivyo ushirikiano wa Jumauia ya Afrika ya Mashariki kutaweza kutoa fursa zaidi kwa nchi hizo kuona maendele zaidi yalipifikiwa katika nchi zao.

Katika ziara yake hiyo aliatembelea shamba la Kizimbani kuaona mazao ya viungo na baadaye alikwenda kuangalia Msitu wa Jozani na Hoteli za Bwejuu amabako alisifu hatua ya wazalendo jinsi walaivyojitokeza kuendeleza biashara katika sekta ya utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.