Kuna matumaini Juhudi za uokoaji meli iliyozama Z’bar zatoa matumaini
Ni baada ya ‘tagi’ kufanikiwa kuiburura kidogo jana
kazi ya uokoaji kufanikiwa
Na Mwantanga Ame--Zanzibar leo,
JUHUDI za uokoaji wa Meli ya MV. Fatihi, iliyozama katika Bandari ya Zanzibar zimefanikiwa kuiondosha kutoka sehemu ilipozama na kuisogeza mbele kidogo.
Hatua hiyo inaleta matumaini ya kuwepo uwezekano wa kurahisisha juhudi za kuibirua ili kuwatafuta maiti waliosalia kwenye meli hiyo.
Meli hiyo ilizama mwishoni mwa wiki iliyopita katika Bandari ya Zanzibar kabla ya kufunga gati na kusababisha watu sita kufariki na wengine 33 kunusurika baada ya kuokolewa.
Kazi ya uokoaji inayowashirikisha Vikosi vya Jeshi la Ulinzi , Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM) na wataalamu mbali mbali jana iliingia siku ya tano huku juhudi zikiendelea.
Usugezwaji wa meli hiyo ulifanywa kwa kutumia ‘tagi’ ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) iliyowasili rasmi kusaidia juhudi hizo za uokoaji kushirikiana na ya Shirika la Bandari Zanzibar.
Hata hivyo, ‘tagi’ hiyo ya TPA ilipata hitilafu na kushindwa kuitunua meli hiyo .
Baada ya mafanikio hayo ya kuisogeza kidogo bidhaa kadhaa zilizokuwemo kwenye ajali hiyo zilishuhudiwa zimetawanyika na kuelea baharini huku kukiwa na harufu kali ya kuhanakiza katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirika la Bandari Zanzibar, Abdi Omar Maalim, alisema kwa kiasi fulani zoezi hilo limeweza kufanikiwa .
Alisema kazi hiyo inafanywa kwa vile bado upo wasiwasi kwamba wapo watu zaidi wanaweza kupatikana kwenye meli hiyo.
Alisema iwapo itashindikana kuenuliwa itabururwa kwa kutumia ‘tagi’ na kuwekwa mbali na eneo la bandari.
Alieleza kwamba hivi sasa baada ya juhudi za siku nne jana kuna dalili kubwa ya kuwepo mafanikio ya kazi za uokoaji kukamilika.
Awali jana Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi akiwemo mkuu wa Jeshi la Polisi Said Mwema na Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), David Mwanyange, walitembelea Bandari hiyo na kuzungumza na Kamati ya Maafa ya Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi, Said Mwema, alisema tukio la kuzama meli hiyo ni la kusikitisha na litoe fundisho kwa Viongozi wa Shirika hilo kuandaa mazingira bora ya kunusuru majanga kama hayo.
Nae Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Jenerali Davis Mwamnyange, aliwataka askari katika kikosi cha uokozi cha JWTZ, chenye wapiganaji 30 kufanya kazi vizuri kwa kuwa ni sehemu ya jukumu lao.
Alisema Askari hapashwi kutumika katika vita pekee na ndio maana jeshi hilo likaitwa ni la wananchi wa tanzania na sehemu ya uokozi katika majanga ni kazi zao.
Hadi tunakwenda mitamboni vikosi vya uokoaji viliendelea na juhudi hizo kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanikiwa haraka iwezekanavyo.
Meli ya Fatihi, ilizama Mei 29, 2009, katika bandari ya Zanzibar ambapo zaidi ya watu sita wanahofiwa kufariki na wengine 33 walinusurika kufa baada ya kubiruka wakati wakiteremka abiria waliokuwa wakitokea Dar es Salaama.

CHANZO - ZANZIBAR LEO
No comments:
Post a Comment