Habari za Punde

KUNA WAKATI WA KUSOMA...

Na pia wakati wa mapumziko ambapo, ingawa kuna mchezo mzuri kwenye T.V, wasichana hawa walionekana kuushughulikia zaidi mchezo wa LUDO katika kupumzisha akili.

Hapa wanaonekana wengine wakijighulisha na mchezo mgumu wa Chess ambao unahitaji kutumia maarifa zaidi na kuona mbali katika uchezaji wake.

Akitafakari acheze move gani hapa na mwenzake tayari ameshajiandaa kukabiliana nae kumnusuru mfalme (king) asije kushambuliwa na kupigwa check mate.


Kilichonifurahisha katika picha hizi ni kuona jinsi gani akinamama wameweza kufikiria kupumzisha akili kwa kujishughulisha na michezo ambayo huhitaji kutumia mbinu na maarifa kuliko kukaa na kupiga soga au muda mwingi kutazama T.V.

1 comment:

  1. Mapara,
    Uwe unatwambia picha hizi zimepigwa eneo gani wakati gani na ikibidi hata majina ya wanaopigwa picha for authenticity reasons, otherwise hizi picha na ujumbe nimezipenda sana.
    mdau Misri.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.