- Kumuomba Allah Subhaanahu Wata’ala Atupe afya njema na nguvu ya kuweza kuukamilisha Mwezi mtukufu wa Ramadhaan.
- Kuusafisha moyo kutokana na wivu , choyo, unafiki, ujeuri na kila maradhi ya moyo.
- Kuhifadhi ulimi, kujiepusha mbali na kusengenya, uongo pamoja na mikusanyiko ya watu isiyokuwa na maana.
- Kuzidisha Dua na Dhikri mbalimbali. Tumia muda wako kwa mambo ya lazima na yenye kukuletea faida.
- Kuwa na mahusiano mazuri na Qur-aan kwa kuisoma, kufuatilia maana na kutekeleza ujumbe uliokusudiwa.
- Kuhakikisha unafaidika na SWAUMU. Chunga akili, moyo, macho, masikio, na viungo vyako vyote kwa ujumla kutokana mambo yote ya HARAAM.
- Ramadhaan ni mwezi wa kuzidisha Ibada, nidhamu na utulivu.
- Ni Mwezi wa Sadaka, mazingatio na kujitolea.
- Katika Mwezi wa Ramadhaan Allah Subhaanahu Wata’ala Hutupa zawadi ya uchamungu, kujiepusha na yaliyokatazwa na kuyafanya yaliyoamrishwa .
- Kuwa pamoja na watu wazuri kwa kuhudhuria madarsa, kusali Sala tano za fardh msikitini, Taraaweh na Sala za usiku.
No comments:
Post a Comment