Habari za Punde

KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA KURA YA MAONI YA UUNDAJI WA SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA ZANZIBAR UKUMBI WA SALAMA BWAWANI.

KATIBU Mkuu wa CUF Seif Sharif Hamad, Mkuu wa kitengo cha Political Press &Project Ubalozi wa Uingereza Mark Polatajko na Political Advisor Pascal Mayalla wakibadilishana mawazo baada ya kutangazwa matokeo ya kura ya maoni.

MWENYEKITI wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande akisoma matokeo ya kura za maoni kwa wananchi katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani.
VIONGOZI wa Vyama vya Siasa wa CUF na CCM, Maalim Seif Sharif Hamadi Katibu Mkuu wa CUF na Saleh Ramadhani Feruoz Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar. baada ya kutangazwa matokeo ya jumla. WANANCHI wakishangilia matokeo ya jumla ya ushindi wa kura ya NDIO. baada ya kutangazwana Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar.
WAANDISHI wa Habari wa Vyombo mbalimbali wakituma habari ndani ya chumba cha kutangazia matokeo katika ukumbi wa salama bwawani.ambayo imefadhiliwa na wahisani wa maendeleo kupitia UNDP kupitia programu ya ESP TANZANIA.
WANANCHI wakishangilia baada ya kutangazwa matokeo ya kura za maoni katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel.
VIONGOZI wa Vyama vya Siasa Zanzibar Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Hamad Khatib Mussa, Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar Saleh Ramadhani Feruoz, Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu na Sera CUF Salum Dimani.
WAPIGA Picha wa vyombo mbalimbali wakiwa makini kupata picha bora katika ukumbi wa Salama Bwawani yakitolewa matokeo ya kura ya maoni.
MTAALAMU wa kutumia ishara kwa Watu wenye ulemavu wa kutokusikia akitowa ishara kwa vitendo katika ukumbi wa Salama Bwawani wakati wa utoaji wa matokeo ya kura za maoni.
WAANGALIZI wa Kimataifa wa uchaguzi wa kura ya maoni Zanzibar wakisikiliza matokeo ya kura za maoni wakati akitowa matokeo hayo Mwenyekiti wa Tumu ya Uchaguzi Zanzibar Khatib Mwinyichande, baada ya kumalizika uchaguzi huo.
WANANCHI wakiwa nje ya ukumbi wa Salama Bwawani wakisikiliza matokeo ya kura za maoni kupitia TV.
Hivi ndivyo ilivyokuwa wakati wa kutowa matokeo ya kura za maoni Zanzibar katika ukumbi wa Salama Bwawani hotel.
Viongozi wa Vyama vya Siasa Zanzibar kushoto Ali Juma Khatib Katibu Mkuu wa TDA, Nassor Khamis wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi akitowa matokeo ya Uchaguzi wa kura ya Maoni katika Ukumbi wa Salama Bwawani Hotel.
Mwandishi wa Gazeti la Zanzibar leo Mwantanga Ame akifuatilia utoaji wa matokeo ya kura ya maoni katika ukumbi wa Salama hoteli ya Bwawani.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.