
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akizungumza na Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Jacque Champagne De Labriolle (kushoto) na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Dianne Corner.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Utanuzi wa barabara ya Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi, Maafisa wa Benki ya Dunia na Viongozi wa Kampuni ya Sogea Satom na Viongozi wa Wafanyakazi wa Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akisalimiana na Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania Diane Corner, anaifutia ni Balozi wa Ufaransa baada ya uzinduzi wa barabara mpya ya kurukia Ndege, iliofanyika katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume. Jina hili limepewa uwanja huo katika sherehe za uzinduzi wake.

VIONGOZI wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Viongozi wa Kampuni iliyojenga barabara mpya ya kurukia Ndege ya Sogea Satom wakiwa katika picha ya pamoja baada kuzinduliwa mradi huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume.
No comments:
Post a Comment