Na Mwandishi wetu
MMOJA wa wajumbe wa Kamati ya watu 14 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Abdalla Said Natepe, amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Mjini Dar es Salaam jana.
Natepe ambaye alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi la kwanza (MBM), ni mmoja wa viongozi walioshiriki kikamilifu katika Mapinduzi hayo yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar kutoka katika utawala wa kikoloni.
Pamoja na kushiriki Mapinduzi hayo, Natepe pia alishika nafasi mbali mbali za uongozi wa juu katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo Waziri wa Nchi Afisi ya Rais.
Aidha Natepe alikuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa ASP na alipokuwa Mzee alikuwa Mshauri mkubwa wa viongozi wa Serikali ya Zanzibar na ile ya Tanzania, pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kifo cha Natepe kinafanya idadi ya Kamati ya watu 14 ya Mapinduzi ya Zanzibar kubakia watu wachache, akiwemo Ramadhan Haji Faki na Hamid Ameir, baada ya wengine kufariki dunia katika vipindi tofauti.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, taarifa ya mazishi ya kiongozi huyo zilikuwa hazijapatikana.
Nimepokea habari ya kifo cha Mzee Abdalla Said Natepe kwa huzuni.
ReplyDeleteNina tuma rambi rambi zangu kwa kupitia Jikumbuke...
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Kwa Familia ya Marehemu
Na Wazanzibari wote kwa jumla.
Mdau
Canada
Innaa Lillaahi Wainnaa ilyahi raajiuuna
ReplyDelete