Habari za Punde

RAIS KARUME AFUTARISHA PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK Amani Abeid Karume,(katikati) akiwa katika futari ya pamoja na Viongozi na wananchi waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba jana. Futari hiyo aliiandaa huko Ikulu ya Chake chake Pemba.


Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakiwa katika futari ya pamoja ilyoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Amani Abeid Karume katika IKulu ya Chake chake jana.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK Amani Abeid Karume akisalimiana a wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba baada ya futari ya Pamoja aliyoiandaa katika Ikulu ya Chakechake jana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj DK Amani Abeid Karume akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Dadi Faki Dadi mara baada ya futari ya pamoja na wananchi aliyoiandaa huko Ikulu ya Chake chake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.