Habari za Punde

RAIS KARUME ZIARANI PEMBA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kangani wilaya ya Mkoani, Pemba alipofika kuangalia maendeleo ya ujenzi wa barabara za Mkoa wa kusini Pemba jana.




Baadhi ya wafanyakazi wa Ujenzi wa Barabara ya Kengeja ,Mtambile inayosimamiwa na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi,wakiwa katika hatua ya uwekaji kifusi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,na Mkewe Mama Shadya Karume,wakisalimiana na wananchi wa kisiwani Pemba jana, akiwa katika ziara ya siku mbili kisiwani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume, akipata maelezo wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa ujenzi wa barabara ya Mtambile, kengeja Mkoa wa Kusini Pemba, akiwa katika ziara ya siku mbili kisiwani humo.
Picha na Ramadhan Othman, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.