Habari za Punde

UZINDUZI WA KAMPENI YA URAIS CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI VIWANJA VYA KOMBA WAPYA RAHALEO

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa Chama cha NCCR-MAGEUZI Haji Ambar Khamis akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa Uzinduzi wa chama chake katika Viwanja vya Komba wapya.


Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa NCCR-MAGEUZI Ali Omar akimtambulisha mgombea Urais wa Zanzibar kwa Wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni Viwanja vya Kombawapya Rahaleo.
Mgombea Mweza wa Urais wa Tanzania wa NCCR-MAGEUZI Ali Omar akimnadi mgombea Urais wa Zanzibar Haji Ambar Khamis wakatika wa uzinduzi wa kampeni katika viwanja vya kombawapya.
Mgombea Ubunge Jimbo la Koani Mohammed Masoud akimtambulisha mgombea wa Jimbo la RAHALEO Leila, katika Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Chama hicho kiwanja cha Kombawapya Rahaleo.
Wananchi wakisikiliza sera za Chama cha NCCR-MAGEUZI katika mkutano wa kampeni ya Urais wa Zanzibar.
Mgombea Ubunge wa Chama cha NCCR-MAGEUZI Jimbo la Magogoni Seif Abdalla akitowa sera za chama chake wakati wa kutambulisha kwa wananchi katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni viwanja vya kombawapya Rahaleo.
Baadhi ya wagombea wa nafasiza Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wakimsikiliza mgombea Urais wa Chama hicho akizinduwa kampeni katika viwanja hivyo.
Wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais wa Chama cha NCCR-MAGEUZI akitowa sera zake katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni ya Urais wa Zanzibar katika kiwanja cha Komba wapya Rahaleo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.