Na Bakari Mussa, Pemba
MGOMBEA mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesifu juhudi zilizochukuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Amani Abeid Karume kwa kusema amefanikiwa kujenga maslahi na mustakbala bora kwa Wazanzibari.
Dk. Bilal aliyasema hayo jana katika viwanja vya skuli ya sekondari Kizimbani kwenye mkutano wa kampeni Jimbo la Gando.
Alisema Rais Karume amefanya makubwa kwa Wazanzibari na mchango wake utaendelea kukumbukwa na kuthaminiwa daima.
Aliwataka wananchi wa Jimbo la Gando kuchagua viongozi wanaoweka mbele maslahi ya Taifa, pamoja na kuijengea heshima Tanzania kwa kusimamia amani na utulivu.
Alisema ngome ya CCM bado iko imara na kwamba kama kitaendelea kubakia madarakani kitaongeza kasi ya kuimarisha maendeleo bila kujali itikadi za kisiasa.
Dk. Bilal amesema hataona aibu katika kusimamia na kudumisha Muungano kwa maslahi ya nchi mbili na serikali zake.
"CCM haitampiga mtu wala kumdanganya, badala yale itaendelea kuimarisha huduma za afya, elimu, kilimo na kujenga maisha bora ya wananchi bila kuwabagua," alisema Dk. Bilal.
Aliwataka wananchi wa Gando kutoendelea kuwachagua wapinzani, ambao wamekuwa wakiwadanganya na kuwarubuni huku wapiga kura wakiwa hawafaidiki na lolote.
Amewaomba wananchi kumchagua Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Rais wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal kuwa Rais wa Zanzibar pamoja na Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kutoka CCM.

No comments:
Post a Comment