Yakamatwa kwenye maduka ya wauza gari
Na Mwantanga Ame
TAARIFA za ukamataji magari ya wizi yaliyoibiwa kupitia mtandao wa kimataifa wa wizi wa magari na kuingizwa Zanzibar, matokeo yake yamefikishwa Makao Makuu ya Polisi jiji Dar es Salaam kwa kufanyiwa kazi zaidi.
Hapo awali jeshi la Polisi nchini kwa ushirikiano na Shirikisho la Polisi la Kimataifa (INTERPOL), lilifanikiwa kukamata jumla ya gari 61 zilizoibiwa katika mbalimbali na kuuzwa nchini kinyemela.
Operesheni hiyo ilifanyika kulingana na vipaumbele vya Mashirikiano ya Majeshi ya Interpol, Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Kusini mwa Afrika na Shirikisho la Majeshi ya Polisi ya Afrika Mashariki.
Naibu Kamishna wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Peter Kivuyo, mwezi uliopita mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam alieleza magari hayo yalikamatwa katika operesheni maalumu iliyopewa jina la MODJADJI, kutokana na kuwapo kwa taarifa za kiintelijensia zilizokusanywa sehemu mbalimbali.
Taarifa za operesheni hiyo ilifahamisha kuwa magari 10 kati hayo yaliyokamatwa katika operesheni ya saa 24 iliyofanyika Agosti 27 na 28, mwaka huu ambapo yalikutwa na kasoro mbalimbali ikiwemo nyaraka za magari ambazo zinatofautiana kwenye chassis.
Magari mengi yaliyokamatwa yalionekana kuibiwa na idadi yake kwenye mabano ni Afrika Kusini (12), Japan (22), Malaysia (8), Uingereza (3) pamoja na Kenya, Australia, Ujerumani , Slovenia , Msumbiji na Tanzania.
Baadhi ya maeneo yaliyoongoza kwa kukamatwa na magari hayo ya wizi kuwa ni Mkoa wa Kinondoni uliongoza kwa kukamatwa gari za wizi (12) ukifuatiwa na Zanzibar (8), Ilala (5) na Mbeya (3).
Tangu kukamatwa kwa gari hizo hadi sasa yaliokamatwa Zanzibar yakiwemo aina Toyota, Nissan bado yapo katika kituo cha Polisi cha Mkoa wa Mjini Magharibi Mwembe Madema yakisubiri khatima yake.
Magari hayo ya Zanzibar, yalikamatwa katika yadi ya Kiembesamaki inayomilikiwa na mfanyabiashara Salim ambapo Polisi hao waliweza kuyatambua baada ya kuyafanyia uchunguzi kutokana na kuwemo katika orodha ya gari zilizoibiwa duniani.
Akizungumza na Zanzibar Leo, Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa, alithibitisha kukamatwa kwa gari hizo na bado zipo Zanzibar taratibu zaidi zinaendelea.
Alisema uchunguzi wa suala hilo hivi sasa umeshakamilika na taarifa zake zinapelekwa Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanyiwa kazi kwani taarifa za kimataifa za upatikanaji wa gari hizo haukuwa Zanzibar pekee.
Kamishna huyo, alifahamisha kuwa wamechukua muda kutokana na magari hayo yalipitia katika njia ndefu baada ya kuibiwa kutokana na wafanyabiashara wa Zanzibar waliokutwa nayo wapo walionunua kutoka Japan kupitia Dubai na kuingizwa Zanzibar.
Hapo awali alisema kabla ya kukamatwa magari hayo walifanya msako wa kuyatafuta barabarani, lakini baada ya kutofanikiwa ndipo walipoamua kuingia katika maduka ya magari ya baadhi ya wafanyabishara wa Zanzibar na kunasa idadi hiyo.
Kamishna huyo alisema kulikuwa na mzunguuko katika kuyapata magari hayo kwani palilazimika pawepo ushirikiano wa wafanyabishara walioingiza gari hizo na kutafuta vielelezo vya kuingizwa nchini.
Alisema baada ya kukamilisha hatua hizo hivi sasa wanasubiri kupata matokeo juu ya suala hilo ambalo linasimamiwa na 'Interpol'.
Tanzania imefanikiwa kunaswa kwa magari hayo baada ya hivi sasa kuwapo kwa ushirikiano wa Askari wa Kimataifa ambapo katika msako huo pia waliweza kuwakamata wahamiaji haramu 42, silaha haramu 13 pamoja na risasi 506. Wahamiaji haramu waliokamatwa ni Wasomali 14, Warundi (24), Wakenya (2), Mzambia mmoja na Mkongo mmoja pamoja aina ya dawa za kulevya zilizokamatwa katika operesheni hiyo kuwa ni Heroin gramu 243, bangi kilo 43.

No comments:
Post a Comment