Na Rajab Mkasaba
JUMUIYA inayojishughulisha na masuala ya afya inyoshirikiana na Chuo Kikuu cha Hopkins cha Marekani, JHPIEGO, ameeleza kuvutiwa kwake na hatua zilizofikiwa Zanzibar katika kuimarisha huduma za sekta ya afya nchini ikiwa ni pamoja na afya za akina mama na watoto.
Akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume, Rais wa JHPIEGO Dk. Leslie Mancuso, aliyasema hayo leo Ikulu mjini Zanzibar.
Katika maelezo yake Dk. Mancuso alimueleza Rais Karume kuwa hatua zilizofikiwa Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ni za kuungwa mkono kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana.
Alieleza kuwa Jumuiya ya JHPIEGO imekuwa na mashirikiano mazuri na Wizara ya Afya kutoa pongezi kwa Wizara hiyo kwa kusimamia vyema programu zinazosimamiwa na Jumuiya yao.
Dk. Mancuso alieleza kuwa JHPIEGO inathamini sana ushirikiano uliopo kati yake na Wizara ya Afya ambao umepelekea kupata mafanikio makubwa katika kuendeleza programu mbali mbali ikiwemo ‘MAISHA Programu (MP)’.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Mancuso alimueleza Rais Karume kuwa Jumuiya hiyo itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake kati yake na Wizara ya Afya kwa malengo ya kuinua sekta ya afya hapa nchini sanjari na kuunga mkono hatua zilizofikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Karume katika sekta hiyo ya afya.
Aidha, Dk. Mancuso alitoa pongezi kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Wizara ya Afya kwa mafanikio makubwa yaliofikiwa katika kupiga vita Malaria na kueleza kuwa mafanikio hayo ni funzo kwa nchi nyengine za ndani na nje ya Zanzibar zinazopambana na Malaria.
Alieleza kuwa kuwepo wka miundombinu bora hapa nchini nako kumechangia kwa kiasi kikubwa kupata mafanikio hayo kwani nchi nyingi duniani hushindwa kupata mafanikio kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu iliyo imara.
Nae Rais Karume kwa upande wake alitoa pongezi kwa kiongozi huyo wa Jumuiya ya JHPIEGO kwa mashirikiano mazuri yanayotolewa na jumuiya yake katika kuimarisha huduma za afya hapa Zabzibar.
Rais Karume alieleza kuwa mafamikio makubwa yameza kufikiwa kutokana na mashirikiano ya pamoja sanjari na juhudi zilizochukuliwa na Seikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Aidha, Rais Karume alisema kuwa huduma za afya imezidi kuimarika hapa nchini kiasi ambacho kila mwananchi hasumbuki kufuata huduma hizo masafa marefu kwani kila baada ya kilomita tano tayari hupatikana kituo cha afya katika maeneo yote hapa Zanzibar.
Alieleza kuwa mbali ya hatua hiyo, kwa upande wa kupiga vita Malaria mafanikio yameweza kufikiwa kutokana na mipango kabambe iliyowekwa na serikali kwa Mashirikiano ya Washirika wa Maendeleo ikiwemo serikali ya Marekani kupitia Mfuko wa Rais Bush na mfuko wa USAID.
Rais Karume alitoa pongezi kwa Serikali ya Maprekani na Jumuiya hiyo kwa kuendeleza kuunga mkono juhudi za Zanzibar katika kuimarisha sekta ya afya ambayo imepiga hatua kubwa na kupayta mafanikio.
Katika maelezo yake, Rais Karume alisema kuwa kuimarishwa kwa miundombinu ya barabara, mawasiliano ya simu na ukaribu wa huduma za afya nako kumechangia kwa kiasi kikubwa kupata mafanikio katika sekta ya afya hasa kupiga vita Malaria.
Rais Karume alisema kuwa mafanikio hayo ndio yaliopelekea na kuchangia katika mapambano ya Malaria hatua ambayo imesaidia hasa katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Mohammed Jidawi alieleza kuwa kutokana na mafanikio yaliopatikana katika kupiga vita Malaria, Zanzibar imeweza kutoa elimu juu ya kupambana na maradhi hayo katika nchi mbali mbali ikiwemo Senegal, Malawi na nchi nyengine za bara la Afrika.
Aidha, Dk. Jidawi alisema kuwa mbali ya nchi hiyo Wizara yake imeweza kutoa wataalamu kwa lengo la kusaidia katika vita ya Malaria huko katika Kanda ya Ziwa maeneo ya Muleba na tayari mafanikio yamepatikana.
JHPIEGO, iliyoaniishwa mwaka 1973, imeweza kufanya kazi zake hapa Zanzibar tangu mwaka 2008 katika programu yake ya ‘MAISHA’ ambapo katika programu hiyo imeweza kupungua vifo vya akina mama na watoto, maambukizi ya virusi vya ukimwi na mambo mengineyo.

No comments:
Post a Comment