
VIONGOZI wa Chama wakisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha Mwanachama wa CCM aliyefariki kwa ajali ya gari akitokea Jambiani kuhudhuria mkutano huo na watu wengine kujeruhiwa katika ajali hiyo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Amani Abeid Karume akisalimiana na Rais Mtaafu wa awamu ya tano Dk. Salmin Amour alipohudhuria katika mkutano wa ufungaji wa kampeni ya CCM kiwanja cha Demokrasia.

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha CCM Dk. Ali Mohammed Shein akisalimiana na Rais Mstaafu wa Awamu ya tano Dk. Salmin Amour, alipowasili kiwanjani hapo.

RAIS Mstaafu Dk Salmin Amour Juma akiwasalimia Wananchi na WanaCCM akiwasili katika Viwanja vya Mkutano wa ufungaji kampeni za CCM.

RAIS Mstaafu Dk. Salimin Amour Juma akisalimiana na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamsi Vuai Nahodha alipowasili katika kiwanja cha Demokrasia.

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika kiwanja cha Demokrasia Kibandamaiti katika Mkutano wa kufunga kampeni ya chama hicho.
Ahsante sana othman mapara, ni hapa tu nimekua nikitegemea ghabari za uchaguzi kutoka kwetu taifa kla znz
ReplyDeleteOsmania