Na Issa Mohammed
NDEGE ndogo imetua barabarani kwa dharura baada ya kupata hitilafu ya mashine yake eneo la Chau nje kidogo ya kijiji cha Mtende wilaya ya kusini Unguja jana.
Akizungumza na Zanzibar leo huko Mtende Meneja Mawasiliano ya Anga Zanzibar, Said Sumry, amesema ndege hiyo ilikuwa ikitumika kwa mafunzo ya urubani.
Alifahamisha kuwa ndege hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Tropical Air ilikuwa ikiendeshwa na rubani Keyvan Cazdat, raia wa Iran, aliyekuwa akimfundisha urubani, Abrahman Mohammed, raia wa Tanzania.
Hatahivyo, alisema rubani huyo pamoja na mwanafunzi wake wako salama, ingawa ndege imepata athari kidogo kutokana na kuingia kwenye msingi wenye mawe.
Alisema ndege hiyo iliruka katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Kiembesamaki nje kidogo ya mji wa Zanzibar, saa 3.44 asubuhi, na ilipofika eneo hilo saa 3.55, ilipata hitilafu ikiwa angani, ndipo rubani akaamua kutua barabarani.
Sumry alieleza ndege hiyo yenye namba 5H-TFS aina ya Piper 28-140, kwa kawaida hutumika kuwapa mazoezi marubani wanafunzi katika eneo hilo, kutokana na kutotumiwa na ndege nyingine zinapofanya safari zake za kawaida.
Tukio la ndege kutua barabarani kwa dharura ni la pili katika kipindi cha mwaka huu, ambapo mapema mwaka huu ndege ndogo kama hiyo ilitua katika barabara ya Kiwengwa mkoa wa Kaskazini Unguja.
Pia ndege ndogo ya kampuni hiyo ya Tropical Air iliwahi kuanguka baharini miaka kadhaa iliyopita karibu na kisiwa cha Chumbe, wilaya ya Kusini Unguja, ikiwa na abiria wawili ambao ni mtu na mkewe.
Katika tukio hilo, abiria hao pamoja na rubani walinusurika kifo baada ya rubani kuwavisha abiria wake vifaa maalum vya kuokoa maisha vilivyowawezesha kuelea baharini, kabla ya ndege hiyo kuanguka.
Rubani na abiria hao waliokolewa baada ya kuelea baharini kwa zaidi ya saa 12
Labels
- .
- `
- 8
- AFYA
- AFYA.
- AJALI
- BIASHARA
- BURUDANI
- DINI
- ELIMU
- FILAMU
- HABARI
- HARUSI
- HOSPITALI
- I
- JAMII
- KATUNI
- Kii
- KILIMO
- KIMATAIFA
- KITAIFA
- Ku
- MAGAZETI
- Mahkamani
- MAISHA
- MAKALA
- MAKALA AFYA.
- MAKALA.
- MATUKIO
- MATUKIO.
- MICHEZO
- MITAANI
- MIUNDOMBINU
- MSAADA
- Ok
- SIASA
- TANGAZO
- TAWA YAWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA UWEKEZAJI
- TEKNOLOJIA
- UCHUMI
- UTAFITI
- UTALII
- VIDEO
- VIJANA
- VISA INTERNATIONAL YAZINDUA TAWI TANZANIANa Mwandishi wetu 16.07.2025DAR ES SALAAM
- WEZI
Tafsiri ya Lugha
Popular Posts
-
Dar es Salaam. 28-10-2025 Tanzania Bloggers Network (TBN) inatoa pongezi za dhati kwa Watanzania wote, wagombea, vyama vya siasa, Tume Huru ...
-
Mtaalamu wa lugha ya Alama Masika Khamis Ali akitoma maelezo kwa Wananchi wa makundi maalumu wakati wa ufungaji wa Mkutano wa Kampeni wa Cha...
-
THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR (SUZA) JOB OPPORTUNITIES The State University of Zanzibar (SUZA) is the only public University in...
-
Msanii wa Bongo Fleva Nandy akiburudisha kwa wimbo wake wa kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein A...
-
Kaimu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu Bw. Bernard Marce...
-
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na hofu ya ulinzi na usalama wao siku ya uchaguzi Oktoba 29, 2025 na limewasihi wakapige kura n...
-
Na Mwandishi Wetu WMJJWM- Njombe Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Mkaundi Maaalum Dkt. John Jingu, amewataka...
-
Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha ADC Mhe.Hamad Rashid Mohammed akisalimia na Viongozi mbalimbali alipowasili katika viwanj...
NDEGE YA KAMPUNI YA TROPICAL YATUA KWA DHARURA BARABARANI KIJIJI CHA MTENDE MAKUNDUCHI.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
BLOGU RAFIKI
-
-
Rais na Mgombea wa nafasi ya Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan apiga Kura katika Kituo cha Ofisi ya Kijiji Chamwino mkoani Dodoma - Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mgombea wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) M...3 days ago
-
Elimu : Bajeti za Elimu Zisipuuzwe wakati wa misukosuko ya Kiuchumi na Kisiasa Duniani - Kikwete na Malala Waonya. - Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Malala Yousafzai, wameonya juu ya mwenendo hatarishi duniani wa kupunguza au ku...2 weeks ago
-
MAHOJIANO YA TAUSI SUEDI NA AMRI NGOYE KUHUSU CSI KUPITIA KWANZA PRODUCTION NCHINI MAREKANI - Pata habari motomoto kupitia facebook kwa kulike huu ukurasa wetu https://www.facebook.com/pages/Pamojapureblogspotcom/312633955485619?ref=hl7 years ago
Marafiki Duniani
Popular Posts
-
Mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili Zanzibar majira ya mchana kwa Ndege na kuendelea na taratibu za Maziko yatafanyika katika Mtaa wa...
-
The United Republic Of Tanzania National Examination Council of Tanzania Form Four Examination Results 2017/2018 The National E...
-
Makamanda wa JWTZ wakiwa wamebeba mwili wa Marehemu Waziri Kiongozi wa Kwanza wa Zanzibar na Brigedia Jenerali Mstaaf Ramadhani Haji Faki...
-
Na Miza Kona/Rahma Khamis Maelezo-Zanzibar Jumla ya wanafunzi 16,744 wamechaguliwa kuendelea masomo ya kidatu cha tatu kati ya wanafun...
-
Bwana Harusi Lusajo Sajent Mwangambaku (kushoto), akiwa katika pozi na mke wake Neema Stanley Matowe katika hafla yake ya ndoa iliyofa...
-
Mama mjazito akihangaika na hatimaye kupoteza maisha kutokana na mimba za utotoni..Video ipo hapo chini baada ya maelezo mafupi
-
Hutuba ya Mhe Waziri wa Afya Nd. Mahmoud Thabit Kombo kwa Waandishi wa Habari Katika Maadhimisho ya Siku ya Malaria Dunia Zanzibar, 22...
-
Madawa na Maji vilivyokabidhiwa na Balozi wa Kuwait Nchini Tanzania Balozi Jasem Al-Najem, kwa Wizara ya Afya kwa ajili ya Kambi za K...

No comments:
Post a Comment