MAKOSA 826 ya jinai, usalama wa barabarani, ajali na mengine mabali yaliasilishwa mahakamani kutolewa maamuzi ambapo 127 wahusika wake waliachiliwa huru kati ya makosa 3,300 yaliyoripotiwa kati ya Januari hadi Septemba mwaka, Kusini Unguja.
Hayo yalibainika jana, wakati Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani humo, Makarani Khamis Ahmed akizungumza na gazeti hili Polisi Mwera jana.
Alisema kutiwa hatiani kwa makosa hayo ni kutokana kupatikana kwa ushahidi na kesi 289 zinaendelea kusilizwa, ambapo baadhi ya kesi watuhumiwa wake wameachiwa huru na kesi nyengine zikiendelea kunguruma mahakamani.
Makarani alisema kulingana na takwimu, kuna upungufu wa makosa 48 kulingana na takwimu za miezi tisa mwaka jana na kipindi kama hicho mwaka huu.
Alieleza makosa yaliyotokea kwa miezi tisa mwaka huu ukilinganisha na kipindi kama hicho mwaka jana, kuna upungufu wa matukio 48, yakilinganishwa na matukio 3,348 yaliripotiwa mwaka 2009.
"Makosa yaliyoripotiwa kwa miezi tisa kwa mwaka huu yalikuwa ni 3,300 kati ya hayo makosa ya jinai 872, usalama wa barabarani 2,264, ajali za barabarani 68 ambapo 17 zimesababisha vifo na watu 87 wamejeruhiwa na kwa mwaka jana yaliongezeka hadi kufikia 3,348", alifafanua SP. Makarani.
Alisema makosa ya jinai ya wizi wa kutumia nguvu yamepungua kutoka 13 miezi tisa ya mwaka jana hadi kufikia manane kipindi kama hicho mwaka huu, uvunjaji wa majengo yamepungua kutoka 127 hadi kufikia 122 na unyang'anyi wa kutumia silaha kosa moja ndilo lililoripotiwa hadi kipindi kama hicho.
Hata hivyo, alifahamisha kuwa, makosa yaliyokataliwa na Polisi baada ya kuonekana ushahidi wake ni mdogo ni 1,653 kati ya makosa 3,300 yaliyoripotiwa miezi tisa mwaka huu.
Makarani alisema kesi nyingi za usalama barabarani zilizojitokeza ni matatizo ya leseni, uvaaji wa vitambulisho na kuzidisha abiria.
Alieleza wizi katika ukanda wa utalii kwa sasa hakuna hata kesi mmoja iliyoripotiwa kwa kipindi hicho kutokana jeshi hilo kuimarisha ulinzi kwa kuweka doria za mara kwa mara.
Alifahamisha kuwa, wizi wa mazao bado ni tatizo katika maeneo ya Kiboje, Machui na Bumbwisudi, ambalo linachangiwa kwa kiasi kikubwa na masheha kutotoa vyeti vya kusafirisha mazao hayo, ambapo inakuwa vigumu wakati wanapofanya zoezi la kukamata bidhaa mbali mbali zinaletwa mjini kwa vile wengi wananchi hawana vyeti hivyo
No comments:
Post a Comment