MAMLAKA ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA), imefuta miradi 250 ya uwekezaji baada ya kushindwa kutimiza masharti ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Salum Khamis Nassor, alieleza hayo hivi karibu mbele ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha, Uchumi na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, ambaye ilifanya ziara kwenye ofisi za mamlaka.
Alisema Mamlaka hiyo imelazimika kuifuta miradi hiyo ya maendeleo baada ya wawekezaji walionyesha nia ya kuwekeza nchini kushindwa kutimiza msharti ya uwekezaji visiwani hapa.
Mkurugenzi huyo alisema mbali ya kuifuta miradi hiyo, kuanzia mwaka 2006 Mamlaka hiyo imeajili miradi 195 yenye jumla ya mtaji wa dola za Marekani 2,330,806,343.27
Alisema baadhi ya miradi hiyo ni ya kilimo, uzalishaji, umeme wa gesi na usambazaji maji, viwanda vidogo, hoteli na mikahawa, mawasiliano, usafiri, miradi ya fedha, elimu, biashara, afya na mambo ya jamii.
Akielezea mafanikio katika sekta ya uwekezaji, Nassor alisema, kiasi cha wananchi 30,000 wamepata ajira tangu kuanzsihwa sekta ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar.
Alisema kiwango hicho kimefikiwa kutokana na kukua kwa huduma za vitega uchumi, sekta binafsi na mchango wa jamii katika uzaliashaji viwandani.
Aidha alifafanua kwamba ajira hiyo pia imechangiwa na vijana wengi kujiajiri katia shughuli mbali mbali zikiwemo za biashara za maduka ya utalii, usafirishaji wa watalii, watembezaji watalii, kilimo cha viungo na biashara ya ushoni, kazi za mikono.
Alisema mafanikio hayo pia yamechangia ongezeko la ukusanyaji wa mapato katika mamlaka hiyo kufikia dola 103,948.10 kutoka mwaa 2008 hadi 2009 ambapo kati ya fedha hizo kuna ziada ya dola 14,318.50.
Akizungumzia miradi iliopo katika maeneo huru, alisema imefikia 37 ambapo 19 kati ya hiyo ipo Maruhubi, saba Fumba na 11 iko Amaan ambapo yote inaendelea na biashara zake na kutoa ajira kwa watu 850 wakiwemo wageni 92.
kilichobaki kwa sasa ni kuanzisha vituo vya kazi ili wananchi wa zanzibar waweze kupata kazi,mfano watu wengi wanaofanya kazi za mahoteli sio wazanzibari ...pili serikali lazima iweke mfuko maalum kwa kukopesha watu wanaotaka kusomea utalii na halafu wakianza kazi wakatwe mapaka pesa zirudi....kadi za mzanzibari apewe anaehusika na zisiwe za kisiasa kwani wenzetu nchi za nje ndo wanavyofanya.kama SMZ wakianzisha hivi itakuwa nafuu kwa wazanzibari wengi
ReplyDelete