Habari za Punde

MICHANGO BADO INAHITAJIKA KUSAFIRISHA VIFAA KWENDA ZANZIBAR

Chukua nafasi yako na kufungua kiungo hiki http://www.interconnection.org/get_recipients.html na kuona misaada ya computers mbali mbali zilizotolewa na mashirika ya misaada hapa Northwest ikiwemo sefrioui Foundation. Hakika tunatakiwa kujifunza na kusoma kwa wengine waliopokea misaada hiyo na baadaye kuangalia nyumbani mazingira gani yaliyopo katika kusaidia Zanzibar na Tanzania.

Nchi nyingi zilizopokea computer zina matatizo ya aina nyingi katika mambo ya jamii lakini pia wametumia fursa ya kupokea hizo computer kama hatua ya awali ili kujenga mazingira bora katika huduma za maendeleo ya technology , interconnection wanafanya research zote za kutuma computer huko afrika na mataifa mengine ya Asia ya kusini na pia Latin America kwa niaba ya mashirika ya kujitolea.

Msingi mkubwa ni kufuata masharti muhimu na nina imani kila mmoja wetu akiweza kuona link hii anaweza kuangalia jee Zanzibar ina sababu ya kupokea computer hizo au haina? Ikiwa Kenya imepokea nchi ambayo ina maendeleo zaidi kuliko Zanzibar au Tanzania kwanini mashirika kama Rotary Club Zanzibar wanashindwa kutoa mashirikiano na Watanzania walio nje katika kusaidia juhudi za kuondoa umaskini katika nchi zetu au Wizara husika kama Elimu kuchagua aina ya misaada ambao wanaona muhimu kwao kutokana na ajenda za kupeana nafasi na pongezi za mtu fulani kutoka nje au mashirika ya kimataifa?

Natoa changamoto kubwa sana kwa ndugu zangu tunaweza kuwa nyuma kama hakuna utendaji wa kujiamini katika kusogeza mbele maisha ya Mtanzania na Mzanzibari kwa ujumla kama Tanzania inaingia katika mfumo huru wa soko katika Afrika ya Mashariki 2012. Hakika Watanzania tunatakiwa kwa njia moja au nyengine kujenga nchi imara na zaidi juu yote ni sekta ya Elimu ambayo inaambatana na ukuaji wa technology katika dunia tunatakiwa kuondoa urasimu mkubwa uliojengeka kwa watanzania waliopo nje na ndani katika mashirikiano yetu kusaidia vizazi vipya katika kuondoa wimbi la umaskini uliokithiri katika jamii huko Nchini kwetu

Nina imani wasomaji wengi wanaweza kunielewa maana ya kuandika kwake nina imani na nchi yangu vizuri sana na wengi kati yenu mna uzalendo wa kutosha katika kusaidia maendeleo ya kiuchumi kwa hiyo tumia fursa ya kuona link hiyo kwa faida yenu na pia kukaa na kuzingatia kwa makini kwanini tunashindwa kujikusanya kusaidia mambo muhimu ya nchi yetu hapa America na hata mataifa ya Ulaya.

Tunatakiwa kuondokana dhana kwamba nchi ni bunge , Rais au Speaker au vyama fulani au chama Fulani. Hakika wananchi wana nafasi kubwa sana kuchangia huduma za maendeleo katika nchi yao hivi sasa Watanzania wengi wamekuwa na malalamiko raia wa kigeni wanachukua nafasi za kazi kama katika sekta ya utalii na watanzania na wazanzibar kuwa washindikizaji jee kuna sababu gani kutokea hayo huko Tanzania na Zanzibar hivi sasa? Sitopenda sana kuwa msemaji lakini lisemwalo lipo kama halipo lipo njiani linakuja

Tumia nafasi yako kujenga nchi yako na kutizama wajibu kama Raia wa Tanzania kwa kuchangia mchango wa dollars 10 na zaidi kuondoa vifaa vyetu hapa seattle hadi Zanzibar mwezi January 2011. Hakika ni dhamana kubwa kwako na nchi yako kwa ujumla.

AHSANTE SANA

AMIN ALLY

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.