Habari za Punde

WADAU HII IMEKAAJE HATA MIEZI MITANO HAIJAFIKA!

MWENYEKITI  wa Azam Said Mohammed akimtambulisha Kocha Stewart Hall kwa waandishi hivi leo.
KLABU ya Azam imeingia mkataba wa miezi 18 na kocha Muingereza Stewart John Hall kwa ajili ya kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu Bara.

Hall alikuwa akiinoa Zanzibar Heroes iliyokuwa ikishirikki michuano ya Chalenji iliyomalizika jumapili na timu ya Taifa ya Bara 'Kilimanjaro Stars' kuutwaa ubingwa.Pamoja na 'kudakwa' Azam Hall pia atakuwa akitoa ushauri katika benchi la ufundi la Zanzibar Heroes.

Kocha Hall alikuwa na mkataba wa miaka mitano na sababu kuu aliyoamua sijui tuite kukatisha au kusitisha mkataba ni kwamba Timu ya Taifa ya Zanzibar kwa mwaka mzima ina michuano mimoja tu inayoshiriki kimataifa nayo ni Chalenji kwa hivyo muda wote atakuwa hana kitu cha kumshughulisha na kumkeep busy.

Sijui wadau mmemfahamu vipi Kocha kwani aliposaini mkataba hakulijua hilo? Au ni sababu huyu Kocha tumeletewa na kampuni binafsi hivyo wana uwezo wa kukatisha mkataba wakati wowote?

Ushauri atakoutoa Hall kwa benchi a ufundi utakuwa na maana gani huku akikabiliwa na majukumu mawili wakati mmoja??

ZFA hebu tuliangalie hili suala hili la kufadhiliwa na kampuni binafsi nasi tukijipanga kwa mipango endelevu na kisha tunalazimishwa tutoe baraka zote. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.