Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Dk Ali Mohammed Shein na Mama Mwema Shein,wakisalimiana na Viongozi wa CCM wilaya ya Mkoani,alipowasili katika Ukumbi wa Mkutano na Viongozi wa Wilaya hiyo jana,akiwa katika zira zake za kuonana na viongozi wa Wilaya 10 za CCM ndani ya Mikoa mitano ya Zanzibar
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wa Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein,alipokutana nao kwa ajili ya kuwashukuru kutokana na Ustahamilivu wao katika Uchaguzi wa Amani na Utulivu Bila ya kuwa na Fujo,na kupelekea ushindi wa CCM
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohammed Shein, akipokea Risala ya wananchi kutoka kwa , Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Mkoani Twalib Bilali, katika Ukumbi wa Umoja ni Nguvu Mkoani Pemba
Makamo Mwenyekiti wa Umoja wanawake wa CCM Bi Asha Bakari Makame, akimtambulisha Waziri wa Ustawi wa Jamii, Maendeleo ya Vijana ,Wanawake na Watoto, Bi Zainab, katika mkutano wa viongozi wa CCM Wilaya ya Mkoani Pemba, wa kuwashukuru wananchi kwa kufanikisha uchaguzi wa Amani na Utulivu na kupelekea ushindi wa CCM,katika ukumbi wa Umoja ni Nguvi Mkoani.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein akiwasalimia viongozi wa Chama cha Mapinduzi,CCM Wilaya ya Mkoani Pemba,wakati Mkutano wa viongozi wa Wilaya hiyo wa kuwashukuru wananchi na wanaCCM, kwa kudumisha amani na Utulivu katika uchaguzi mkuu uliopita, katika ukumbi wa umoja ni nguvu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein akizungumza na Viongozi wa CCM Wilaya ya Mkoani kisiwani Pemba.
Picha na Ramadhan Othman, Pemba
No comments:
Post a Comment