Na Aziz Simai Pemba
WATAALAMU wa Kilimo na Mifugo, Kisiwani Pemba, wametakiwa kuwa karibu na Wadau wao kwa kuongeza ushirikiano kwa kubadilishana utaalamu wa Shughuli za kukuza kipato.
Hayo yameelezwa na Mratibu Jumuia ya maendeleo ya ufugaji Pemba, (POFADEO), Omar Hamad Mjaka , huko Kisiwani Pemba wakati alipokuwa akizungumza na Kmati za Shehia za Wawi, Ziwani, Ng’ambwa, Mgogoni, Pujini Mkoroshoni m Matale na Vitongoji kuhusu utekelezaji sheria zinazohusiana na mifugo
Mratibu huyo alisema bado wafugaji wengi wanawafanyia ukatili wanyama wao kiasi cha kutuia huzuni, jambo ambalo nikinyume na sheria za Mifugo.
Alieleza kuwa Sera ya mifugo ya mwaka 2002 inakusudia kuwapa taaluma zaidi ya ufugaji na kuondokana na ufugaji wa zamani usiokuwa na tija kwa mkulima, kuepuka mateso kwa wanyama.
Hivyo alieleza kuwa Jumuiya hiyo itaendelea na juhudi zake za kutowa elimu kwa wafugaji kuwawezesha kujua sheria ya usimamizi wa wanyama na sera ya mifugo ya mwaka 2002.
No comments:
Post a Comment