WAWAKILISHI wa Zanzibar kwenye Ligi ya Mabingwa barani Afrika klabu ya Zanzibar Ocean View, leo wanajitupa katika uwanja wa Martire, kumenyana na AS Vita katika mchezo wa marudiano.
Zanzibar Ocean inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya kuanzia magoli 2-2 ili iweze kusonga mbele katika kinyang’anyiro hicho.
Itakumbukwa katika mchezo wa kwanza Januari 30, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 katika uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.
Kikosi cha timu hiyo kiliondoka juzi na kiliwasili jana mjini Kinshasa ambapo kimefikia katika hoteli ya Emvemsti, baada ya kusota kwa saa moja na nusu kwenye uwanja wa ndege, ambapo wenyeji wao walidai hawakuwa na taarifa za kuwasili kwa timu hiyo.
Zanzibar Ocean View inanolewa na kocha wa timu za taifa za vijana Abdelfatah Abbas akisaidiana na Said Omar Kwimbi, ambapo walipoondoka hapa, waliahidi kucheza kwa kutafuta ushindi ili kuweza kuingia hatua ijayo.
Nao KMKM wanaopeperusha bendera katika Kombe la Shirikisho, jana walitarajiwa kurudiana na DC Motema Pembe mjini humo.
KMKM ikiwa nyuma kwa magoli 4-0 baada ya kufungwa kwenye uwanja wa Amaan, ilikuwa ikihitaji ushindi wa magoli 5-0 kuweza kuwatoa Wakongomani hao
No comments:
Post a Comment