UMOJA wa waTanzania waliosoma Japan (JACA), umefanya uchaguzi mkuu wa mwaka wa kuwachagua viongozi wao wa Kitaifa.
Katika mkutano uliofanyika hoteli ya Cort Yard jijini Dares-saalam ulihudhuriwa na wajumbe 52 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na Zanzibar.
Mkutano huo ulimrejesha madarakani Mwenyekiti wake wa zamani Dk. Zakaria Mgamirwa, baada ya kukosa mpinzani katika uchaguzi huo.
Wengine waliorudi madarakani ni Makamu Mwenyekiti, Peter Mateso, nafasi ya Katibu wa Umoja huo imeshikiliwa na Egina Ngerangeza ambapo Omar Kassim Omar kutoka Zanzibar University alishika nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu na kufanikiwa kumbwaga Twaha Twaha.
Mwanadada Zuhura Makinjinjwa alifanikiwa bila kupingwa kuichukua nafasi ya mtunza hazina wa umoja huo.
Katika nafasi ya wajumbe wanne wa kamati, Hamad Mkubwa kutoka Zanzibar ambae hakuwepo katika uchaguzi huo aliibuka kidedea baada ya mjumbe mmoja Egina Ngizarera kuwa Meneja Kampeni wake.
Wajumbe wengine walioshinda Jakoub Katanga, Dk.Severing Senga, Mudrik Fadhil Abas, Isaya Nangai na wote hao watakaa madarakani mwaka mmoja kwa mujibu wa Katiba ya umoja huo.
Uchaguzi huo Mkuu umesimamiwa na Shirika la Misaada la Japan (JICA).
No comments:
Post a Comment