SHEKH Mussa Salah akiongoza kisomo cha Duwa ya kuitakia Amani na Utulivu wa Mabalaa kisomo hicho kimefanyika katika Viwanja vya Maisara na kuhudhuriwa na Waislamu wa Madhehebu mbalimbali ya Dini ya Kiislam.
KATIBU wa Afisi ya Mufti Zanzibar Fadhil Soraga akitowa neno la shukrani kwa waandaaji wa duwa hiyo na uitikio wa Waislamu kuhudhuria kwa wingi katika Viwanja hiyo.
SHEKH. Ally Bassaleh akisoma risala maalum kwa waislamu waliohudhuria katika kusoma Duwa ya kuitakia Amani na Utulivu Zanzibar na Mabalaa, iliofanyika Viwanja cha Maisara.
Shekh Juma Othman akisoma Quran ya ufunguzi wa kisomo cha duwa ya kuitakima Amani Zanzibar baada ya kufanyika uchaguzi ulio salama bila ya fujo.
SHEKH. Habibu Ali Kombo akisoma Duwa ya Ufunguzi wa Duwa ya pamoja ya Waislamu wa Zanzibar kuitakia mema Nchi na Amani.
SHEKH Hassan Issa akitowa utngulizi kwa Waumini wa Dini ya kiislamu utaratibu wa kusomwa Duwa.
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakisali sala ya pamoja ya Alasir ili kuomba duwa ya kuitakia Amani Nchi na Mabalaa ya Dunia iliyofanyika Uwanja wa Maisara.
VIONGOZI wa Serikali na Dini wakimsikiliza msoma Quran wakati wa kuiombea duwa ya Amani Zanzibar.
WAUMINI wa Kiislamu wakisali sala ya sunna katika viwanja vya maisara.
WAUMINI wa Dini ya Kiislam wakishiriki duwa ya kuiombea Nchi Amani na Mabalaa iliyofanyika katika Viwanja vya Maisara baada ya Sala ya Laasiri.
No comments:
Post a Comment