WATOTO wa Marehemu wakiwa mbele wakiusindikiza mwili wa baba yao baada ya kumalizika kwa ibada iliofanyika katika Kanisa la Anglikana Mbweni, baada ya kufanyika ibada ya mazishi.
WANANCHI wakibeba jeneza baada ya kumalizika kwa ibada ya kumuombea WAUMINI wa Madhehebu ya Anglikana wakiwa katika Misa ya kuuombea Mwili wa Marehemu Joseph Asama katika kanisa la Anglikana Mbweni.
WANANCHI walioudhuria misa ya kuuombea Mwili wa Marehemu wakiwa kanisani Mbweni. Jaji Augustino Ramadhani pia alikuwepo
WAUMINI wa madhehebu ya Anglikana Zanzibar wakifuatilia Misa ya kuuombea Mwili wa Marehemu Joseph Asama
MWILI marehemu Joseph Asama ukiwa katika Kanisa la Anglikana Mbweni ukiombewa katika Misa ya Maziko kanisani hapo.
WAUMINI wakiuweka mwili wa Marehemu Joseph Asama kaburini tayari kwa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
ASKOFU Mstaafu wa Kanisa la Anglikana John Ramadhani mwenye kitabu akiongoza maziko ya Joseph Asama katika Makaburi ya Mwanakwerekwe.
MKE wa Marehemu Joseph Asama Beatrice Asama akiweka mchanga katika kaburi baada ya kuwekwa mwili wa marehemu.
BAADHI ya Waumini wa Madhehebu mbalimbali wakishiriki katika mazishi ya Marehemu Joseph Asama katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
WANANCHI wakiwa na nyuso za simanzi wakati wa mazishi katika viwanja vya makaburi ya Mwanakwerekwe.
HIVI ndivyo ilivyokuwa wakati wa mazishi ya marehemu Joseph Asama Mwandishi na mwanahabari wa siku nyingi Zanzibar
WANAFAMILIA wakiwa na nyuso za simanzi kwa kifo cha ndugu yao wakiwa katika makaburi wakati wa mazishi.
MKE wa marehemu Joseph Asama,Bi Beatrice Asama akiweka shada la maua katika kaburi. MAMA mdogo wa marehemu Brigita Ramadhani akiweka shada la maua kwa niaba ya familia yake.
MKURUGENZI wa Shirika la Utangazaji Zanzibar, STZ Rafii Haji na kushoto na Mtangazaji Gwiji wa STZ Suleiman Juma Kimea wakiweka shada la maua kwa niaba ya Wafanyakazi wa STZ.
JAJI Mkuu Mstaafu wa Tanzania Agustino Ramadhani akisoma risala ya wasifu wa marehemu baada ya kumalizika maziko katika makaburi ya Mwanakwerekwe.
broda ...Nimefeel kama i was there kumzika baba- mkubwa/babu ...but umbali umenifanya nisiwepo...Asante kwako...let da soul of him Rest In Peace
ReplyDelete