Habari za Punde

MJI MKONGWE KUNAFUKUTA...

LEO baada tu ya mvua ya saa nne asubuhi wachina wawili walionekana wanabandika matangazo ya rangi ya mamlaka ya mji mkongwe katika sehemu iliyokuwa uwanja wa mji mkongwe na starehe club. Tangazo moja la upande wa starehe linaarifu kuwa mamlaka ya mji mkongwe imeamua kuruhusu ujenzi wa hoteli ya nyota 5 na kuwataka wananchi watoe maoni yao kuhusu azma hiyo kwa wiki 3 kuanzia tarehe 08.04.2011. leo ni tarehe 19.04. 20011 hivyo wiki mbili tayari zimepita hivyo kuna wiki tu kuwasilisha maoni.

Pili tangazo linalohusu sehemu ya bustani halijaiinishwa vyovyote kuhusisna na tarehe ya kupokea maoni.

Yanayojitokeza:

1. Kwa nini tangazo litoke wiki mbili baada ya kuamriwa kutolewa maoni?

2. Iweje wachina ndio wabandike kibao na si mamlaka ya mji mkongwe ambayo ndio inayo mamlaka wa kufanya hili?

3.Iweje kujengwe hoteli katika eneo ambalo tayari kuna hoteli si chini ya 10 katika eneo moja lisilopungua mita 50 na kusababisha upungufu wa huduma za jamii kwa mfano maji kwa sababu ya matumizi makubwa ya hoteli wakati kuna eneo kama la bwawani ambalo ni kubwa na lingestahili kabisa kujengwa hoteli au kuimarishwa ikawa kweli fahari ya Zanzibar?

4. Iweje itolewe moja ya sehemu za hifadhi kwa ajili ya hoteli ama biashara badala ya kuendeleza hifadhi na urithi wa visiwa hivi.

5. Iweje mpaka leo hakuna mchoro rasmi unaotueleza kinachotarajiwa kufanyika tukaelewa sehemu ipi ndio bustani na ipi ni hoteli.

6. Kama moja ni sehemu ya wazi kwa nini izingiriwe kwa vile ile ni sehemu ya jamii?

Tafadhali, usipuuzie wala kupoteza muda. chukua hatua tuhahkikishe kuwa barua nyingi znaandikwa na kupelekwe shemu zote zinakostahili ikiwemo:

1. Waziri, wizara ya ardhi, makaazi, maji na nishati,

2. Mkurugenzi mkuu, mamlaka ya hifadhi na uendelezaji mji mkongwe, p.o.box 4233 zanzibar, fax. +255242230046 email: stonetwown@zanlink.com

3. Zipa

4. Wizara inayoshughulikia masuala ya mazingira

5. Mwenyekiti, bodi ya mamlaka ya hifadhi na uendelezaji mji mkongwe, p.o.box 4233 zanzibar, fax. +255242230046 email: stonetwown@zanlink.com

kama yupo mwenye anuani zao kamili zisamabazwe.



Tusipuuzie hili jambo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.