WANACHAMA 17 wa UVCCM, wamejitosa kuwania kinyang’anyiro cha uenyekiti wa UVCCM Taifa, huku watano kati yao wakirejesha fomu hadi jana.
Akizungumza na gazeti hili, Katibu Msaidizi Mkuu wa Siasa na Organization UVCCM, Shara Ame Ahmed, alisema vijana hao wamejitosa kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza na gazeti hili, katika ofisi za UVCCM Gymkana mjini hapa Shara waliwataja vijana hao kuwa ni Sadifa Juma Khamis (Mbunge wa Donge), Khadija Nassor Abdi, Shinuna Kombo Juma, Bakari Ali Bakari na Omar Mmadi Muarabu ambayo tayari wamesharejesha fomu.
Wengine waliochukua fomu ni Thabit Jecha Thabit, Hamid Bilal Gharib, Mwanawewe Ussi Yahya, Laila Burhan Ngozi, Rashid Simai, na Mbarouk Mrakib.
Wengine ni Issa Haji Ussi (Mwakilishi wa jimbo la Chwaka), Bimkubwa Sukwa Said, Rahma Khamis Mzee na Omar Justus Moris (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mjini).
Alisema siku ya mwisho wa uchukuaji wa fomu na urejeshaji ni leo saa 10 jioni, ambapo alitoa wito kwa wanaCCM waliochukuwa fomu wawahi kuzirejesha kabla ya muda haujamaliza.
Nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa ya UVCCM unawaniwa baada ya mwenyekiti wake Hamad Masauni kujiuzulu wadhifa huo na kusababisha kuwa wazi kwa kipindi chote tokea mwishoni mwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment