MANDHARI ya mitaa ya Chakechake ikiwa katika harakati za kuboresha maeneo ya mji huo kwa kuendeleza ujenzi wa kisasa, kama wanawavyoonekana wananchi hao wakiondowa kifusi baada ya kubomowa jengo la zamani na kupisha ujenzi wa jengo jipya ili kuboresha mandhari hiyo
WAFANYABIASHARA ya Matunda na bidhaa mbalimbali katika Soko la Chakechake wakifanya biashara zao kwa hali ya wasiwasikutokana na kuwa na karibu na Transfoma ya umeme ilioko kwa muda mrefu chiniyao ikiwa na baadhi ya waya zikiwa karibu na meza zao za biashara, taasi husika inabidi kuchukuwa hali yataadhari na hali hiyo WANANCHI wakiwa katika harakati za kujipatia mahitaji yao kama walivyokutwa wakiwa katika harakati za kujichagulia viatu maarufu katika maeneo ya kilimatinde Chakechake
MJASIRIAMALI wa Biashara ya nguo za Mitumba akitayarisha bidhaa hiyo ili kuweka sawa kwa wateja wake wanofika kuchagua bidhaa hiyo, ambayo hutumika na watu wengi kutokana na ubora wake.
USAFIRI wa gari la Ngombe ni moja ya usafiri unaotumika kwa wingi Kisiwani Pemba na hutowa huduma ya uchukuzi wa mizigo kwa kutumia usafiri huo, moja ya gari la Ngombe likiwa ni mizigo likikatisha mitaa ya Chakechake.
WACHUUZI wa Samaki wa aina ya kamba katika soko la Chakechake wakipanga kamba kwa ajili ya wateja wao wanaohitaji bidhaa hiyo. Fungu moja la Kamba huuzwa shillingi 500/ -
MOJA ya mitaa ya maeneo ya Chakechake unavyokuwa wakati wa saa za kazi ukiwa katika harakati za hapa na pale unavyokuwa na pirikapirika kama wakaazi wanavyonekana pichani
MFANYABIASHARA ndogondogo katika mitaa ya Chakechake akifanya biashara kando ya barabara inayoelekea sokoni chakechake bila ya kujali usalama wake katika eneo hilo akifanya shughuli yake ya kupanga kaseti za Video na huku gari inapita nyuma yake, ikiwa eneo hilo haliruhusiwi kufanya biashara
No comments:
Post a Comment