Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Waziri wa Habari,Utamaduni na Michezo Abdilah Jihadi Hassan,alipotembelea Kituo cha Redio Jamii huko Micheweni Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya hiyo na kuona mambo mbali mbali ya maendeleo
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi wakiwemo pia wanafunzi, katika eneo la kwale gongo, alipotembelea barabara ya Konde-Wete, akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuona mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha wageni, akiwa na Mkewe Mama Mwanamwema Shein,wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya,(Chwaka) Wilaya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi,Group Six Internatinal LTD, Janson Huang,kutoka China, alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Wilaya,(Chwaka) Wilaya Micheweni,Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi na wakulima wa Bonde la Mpunga la Kunambe Darajani, akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya ya Micheweni,Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuona mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
PIcha hii inaonesha sehemu ya Bonde la Mpunga la Mziwanda, ambako wakulima wa bonde hilo wamekumbwa na tatizo la kukosa mavuno kutokana na mashamba kuingiliwa na Maji chumvi,hiyo imetokana na uharibifu wa Mazingira. Sehemu hii pia Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein aliitembelea na kuwapa matumaini mazuri wakulima katika eneo hilo.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akifuatana na Waziri wa Fedha,Uchumi na Maendeleo Omar Yussuf Mzee na Waziri wa kilimo na Maliasili Mansour Yusuf Himid,alipotembelea Bonde la Mpunga la Mziwanda,Wilaya ya Micheweni,Mkoa wa Kaskazini Pemba, akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya hiyo na kuona mambo mbali mbali ya kimaendeleo.
Picha na Ramadhan Othman , Pemba
No comments:
Post a Comment