· Mahakama Kuu ilimuondolea adhabu ya kifungo cha maisha
· Adaiwa kuwafanyia unyama huo watoto wawili
· Pia akabiliwa na kesi mbili za kubaka
Na Mwandishi Wetu
KIJANA wa miaka 22 anayedaiwa kuwa mtu maarufu wa vitendo vya kuwalawiti watoto wadogo wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 15, amefikishwa tena mahakamani kwa shitaka la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11.
· Adaiwa kuwafanyia unyama huo watoto wawili
· Pia akabiliwa na kesi mbili za kubaka
Na Mwandishi Wetu
KIJANA wa miaka 22 anayedaiwa kuwa mtu maarufu wa vitendo vya kuwalawiti watoto wadogo wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 15, amefikishwa tena mahakamani kwa shitaka la kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11.
Mshitakiwa huyo Mohammed Hamza Mohammed mkaazi wa Kiponda wilaya ya Mjini Unguja, amefikishwa mbele ya hakimu Makame Mshamba Simgeni wa mahakama ya mkoa Vuga kujibu shitaka hilo.
Shitaka hilo liliwasilishwa mahakamani hapo na Mwendesha Mashitaka Aziza Idd Suweid, Mwanasheria wa serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Akiwa mahakamani hapo, Mwanasheria huyo wa serikali alimsomea mshitakiwa huyo shitaka hilo ambalo alilikana.
Katika madai yake Aziza alidai kuwa, kinyume na kifungu cha 132 (1) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, mshitakiwa huyo alimuingilia kinyume cha maumbile mtoto wa kiume wa miaka 11 (jina tunamuhifadhi).
Alifahamisha kuwa tukio hilo lilidaiwa kutokea Jang'ombe wilaya ya Mjini Unguja, majira ya saa 1:00 za usiku wa Mei 26 mwaka huu.
Alifahamisha kuwa siku hiyo alimvua nguo mtoto huyo na kumuingiza uume wake katika sehemu zake za siri za nyuma.
Mahakama ilipomtaka mshitakiwa huyo kujibu shitaka hilo alilikana, na kuamua kumpeleka rumande kwa muda wa siku 13 baada ya kumkatalia ombi lake la dhamana.
Pamoja na hatua hiyo ya mahakama, upande wa mashitaka kwa upande wake uliiomba mahakama hiyo kuliahirisha shauri hilo na kulipangia tarehe nyengine kwa ajili ya kutajwa, kutokana na upelelezi wake bado haujakamilika.
Hakimu Makame Mshamba Simgeni alikubaliana na hoja hizo, na kuliahirisha hadi Juni 16 mwaka huu kwa kutajwa.
Sambamba na kesi hiyo, katika mahakama hiyo ya mkoa iliyo chini ya hakimu Hamisa Suleiman Hemed, Mohammed Hamza Mohammed anakabiliwa na kesi nyengine kama hiyo ya kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 10.
Katika kesi hiyo ambayo inategemewa kufikishwa tena mahakamani Juni 9 mwaka huu, kinyume na kifungu cha 130 (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar, alidaiwa kumtorosha mtoto huyo wa kiume kwa kumtoa nyumbani kwao bila ya idhini ya wazazi wake.
Sambamba na shitaka hilo pia alidaiwa kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto huyo (jina tunamuhifadhi), tukio ambalo lilidaiwa kutokea Mfereji wa Wima wilaya ya Mjini Unguja majira ya saa 11:00 za jioni ya Mei 7 mwaka jana.
Mnamo mwaka 2008 takriban miaka miwili na nusu iliyopita, mshitakiwa huyo wakari akiwa mwanafunzi wa kidato cha sita katika skuli ya sekondari ya Lumumba aliwahi kuhukumiwa kifungo cha maisha Chuo cha Mafunzo kwa kosa kama hilo la kumlawiti mtoto mdogo wa kiume.
Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama hiyo ya mkoa Vuga iliyokuwa chini ya hakimu George Joseph Kazi, baada ya kuridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao uliweza kuthibitisha kosa hilo dhidi yake pasi na kuacha hata chembe ya shaka ya maana.
Lakini hata hivyo, adhabu hiyo ilitenguliwa na kuachiliwa huru na Jaji Omar Othman Makungu wakati huo akiwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar, dhidi ya rufaa aliyoiwasilisha mahakamani hapo ya kupinga adhabu hiyo iliyotolewa na mahakama hiyo ya mkoa.
Wakati huo huo, huku akiwa anatumikia kifungo hicho cha maisha chuo cha Mafunzo, Mohammed Hamza pia alikuwa akikabiliwa na shitaka jengine la kumuingilia kinyume cha maumbile mtoto wa kiume, kesi ambayo ilikuwa mbele ya hakimu Hamisa Suleiman Hemed.
Hata hivyo mahakama hiyo iliamua kuiondosha kesi hiyo mahakamani hapo chini ya kifungu cha 209 cha sheria za mwenendo wa jinai (CPA) namba 7/2004 sheria za Zanzibar, baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kusikilizwa mashahidi.
Matukio hayo mawili ya kuwaingilia watoto hao wa kiume, yalidaiwa kutokea siku tofauti katika maeneo ya Chukwani na Bububu wilaya ya Magharibi Unguja.
Kwa mujibu wa kifungu hicho, shitaka lolote lenye dhamana litalazimika kusikilizwa ndani ya kipindi cha miezi minne, na endapo upande wa mashitaka utashindwa kuwasilisha mashahidi ndani ya muda huo, mahakama imepewa uwezo wa kuiondosha kesi hiyo mahakamani.
No comments:
Post a Comment