Mshauri wa Masuala ya Utawala kwa nchi za Afrika ya Mashariki-Sekritarieti Jumuiya ya Madola-London, Dunstan Maina,akitoa mada ya Dhana ya Uongozi kwa Watendaji wa Taasisi mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,wakati wa semina iliyomalizika jana katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort,Nje ya Mji wa Zanzibar.
Jaji Mshibe Bakari wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, pia Mwenyekiti wa tume kurekebisha Sheria,akichangia mada katika semina ya siku tatu kwa watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,inayoendelea katka ukmbi wa Mikutano Zanzibar Beach Resort
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohammed Shein, akiwa mwenyekiti wa Semina ya Uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,kwa watendaji wa Taasisi na Idara mbali mbali,akifafanua jambo alipokuwa akiendesha semina hiyo,iliyojadili Mada mbali mbali zilizotolewa wakati semina hiyo ya siku tatu ikiendelea katika ukumbi wa Zanzibar Beach Resort.
Picha na Ramadhan Othman, Ikulu
No comments:
Post a Comment