Habari za Punde

MABADILIKO MAKUBWA SHIRIKA LA MELI

·      Bandari,Viwanja vya ndege kukusanya mabilioni
Na HalimaAbdalla

WAZIRI waMiundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad amesema  Wizara yake inakusudia kufanya maamuzi yakubadili meli zilizopo ambazo zimepitwa na wakati na kuziuza na kununua melinyengine zitakazoweza kuhimili ushindani wa soko.

Alisemapia kutaanzishwa ajira ya mkataba kwa mabaharia wa meli zilizopo nchini pamojana kukamilisha sheria ya uanzishwaji upya wa shirika la Meli na wakala.

WaziriMasoud alisema hayo wakati akiwasilisha hotuba ya Makadirio ya Mapato namatumzi ya Wizara MiundoMbinu na Mawasiliano kwa mwaka 2011/2012 katika kikaocha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kinachoendelea.

Aidha,alisema kwa mwaka 2011/2012 Shirika la Bandari linategemea kuteremsha nakupakia kiasi cha tani 100,000 za mizigo mchanganyiko pamoja na makontena30,000.

Alisemakwa upande wa miradi ya maendeleo shirika linatarajia kuendelea na uimarishajiwa huduma na rasilimali zake kwa kuimarisha miradi iliyoanzishwa mwaka wa fedhaunaomalizika ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vifaa vya kufanyia kazi bandarini naununuzi wa taa za Solar kwa minara na maboya Unguja na Pemba.

Sambambana hayo, alisema Shirika linatarajia kukusanya shilingi bilioni 9.3 katikakipindi cha Julai 2011 hadi Juni 2012 katika kutekeleza malengo hayo shirika,limepanga kutumia shilingi 6.5 billioni kwa kazi za kawaida.

Aidha,alisema kwa mwaka 2011/2012 Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kupitia Idaraya ujenzi na utunzaji barabara inakusudia kutekeleza na kusimamia miradi mbalimbali ya ujenzi wa Barabara iliyopangiwa.

AlisemaIdara kupitia mfuko wa barabara itaendelea kuzitunza na kuzifanyia matengenezobarabara mbali mbali za mijini na vijijini Unguja na Pemba, ili zipitike mudawote kwa lengo la kuwarahisishia wananchi usafiri.

Aidha,alisema Idara ya usafiri na leseni katika kipindi cha mwaka wa fedha 2011/2012itachukua hatua mbadala kuimarisha usalama barabarani ikiwemo kuendeleakuwapatia elimu watumiaji wa barabara na kuimarisha ukaguzi wa vyombo vya moto.

Alisemahatua pia zitachukuliwa kuhakikisha kuwa karakana kuu ya Unguja na sehemu yamitambo Pemba zinaimarishwa kwa kupatiwa vifaa na wafanyakazi wenye ujuzi nateknolojia ya kisasa ya vyombo vya moto.

Alielezakuwa mwaka 2011/2012 Idara ya usafiri na leseni inatarajia kukusanya jumla yashilingi milioni 280,600,000 na inaombewa jumla ya shilingi milioni370,000,000,kwa matumizi ya kazi za kawaida.

Sambambana hayo, alisema katika kipindi cha mwaka 2011/2012 Mamlaka ya viwanja vyandege inatarajia kukusanya shilingi bilioni 1,210 410,000 kutekeleza shughulizake kama ilivyopangiwa.

Mamlakajiyo imeombewa shilingi milioni 806,000,000 kwa ajili ya kazi za kawaida.

Kwaupande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Mawasiliano na Ujenzi ya Baraza laWawakilishi, Makame Mshimba Mbarouk, aliipongeza Wizara hiyo kwa hatua iliyofikiaya ujenzi wa barabara.

Alisemahiyo inajumuisha miradi ya Barabara mbali mbali inayofadhiliwa na washirika wamaendeleo na Serikali pamoja na barabara zinazofanyiwa matengenezo chini yausimamizi wa Idara ya ujenzi na utunzaji wa barabara kwa fedha kutoka mfuko wabarabara.

Mshimbaalisema hayo alipokuwa akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo ya Makadirio yaMatumizi ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2011/2012.

Alisemabandari zimekuwa zikikusanya mapato kutokana na vyanzo mbali mbali inayopitishwakatika bandari hizo, lakini muhimu zaidi zimekuwa mlango unaotumika kama chanzocha kukusanyia mapato kwa Idara nyengine kama vile Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) na Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.