MAMIA ya wananchi wa Zanzibar na vitongojivyake, jana walihudhuria maziko ya Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM,mzee Masoud Sururu, aliyezikwa kijijini kwao Kiombamvua, Wilaya ya Kaskazini‘B’, Mkoa wa Kaskazini, Unguja.
Maziko hayo yaliongozwa na Makamu Mwenyekitiwa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia ni Rais (Mstaafu) wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume.
Aidha, viongozi wengine wa chama na serikali walihudhuriaikiwa ni pamoja na Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Waziriwa Nchi (OMPR), Mohamed Aboud Mohamed,baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM na viongozi mbali mbali wa CCM wa Mikoa mitatu ya Unguja.
Marehemu Sururu (89), alifariki dunia usiku wakuamkia jana katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) - Lugalo, mjini Dares Salaam, baada ya kuugua maradhi ya kiharusi kwa muda mfupi.
Wakati wa harakati za siasa, marehemu Sururu,alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa ASP katika miaka 1957, ambapo alibahatikakushika nyadhifa kadhaa ndani ya chama na serikali ikiwemo Mwenyekiti wa Tawila ASP Mangapwani na Jimbo la Bumbwini, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ASP naCCM, Ubunge pamoja na Mjumbe wa Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM, wadhifaalioushikilia hadi kufariki kwake.
Chama Cha Mapinduzi kimepokea kwa mshituko,huzuni na masikitiko makubwa taarifa yakifo cha mzee Sururu, kwani kimekuja wakati huu chama hicho kikiwa kimo katika harakati za kuleta mageuzi ya kiuongozina Kiutendaji, ambapo hekima, busara na mchango wake, ulikuwa bado unahitajikakatika kukijenga na kukiimarisha.
Hivyo, CCM imesema daima itamkumbuka marehemuSururu, kutokana na ujasiri, uadilifu, ukaribu wake na watu wa rika na jinsiazote na kubwa zaidi alikuwa ni miongoni mwa wana CCM walioadiriki kutoaushauri, nasaha, maelekezo katika masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi siotu kwa maslahi ya chama, bali pia kwa taifa na wananchi wake.
Chama Cha Mapinduzi kimesema kinaungana nawanafamilia, ndugu na jamaa wa marehemu wa mzee Sururu hasa katika kipindi hikikigumu cha maombolezo na kwamba kinawaomba wawe na moyo wa subra kwa kuondokewana mpendwa wa huyo.
Marehemu mzee Masoud Sururu Jumanne, ameachavizuka wawili , watoto 14 na wajukuu kadhaa.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pemaPeponi, Amiin.
mimi ni munir ambae ni mjuukuu wa mzee masoud sururu na na ina muombea kila la kheri na Mwenyezi mungu ampe wepesi na nuru katika makaazi yake hayo ambayo sisi sote tuko njiani tunakwenda huko huko aamiin.
ReplyDelete