Habari za Punde

MAMA MWANAMWEMA SHEIN AWATEMBELEA WATOTO YATIMA WA SOS NA NYUMBA YA WATOTO YATIMA MAZIZINI.


 MKURUGENZI wa Kijiji cha Watoto cha SOS, Suleiman Mahmoud Jabir akisalimiana na Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mwanamwema Shein alipofika kuwatembelea katika makaazi yao na kuwapa mkono wa Idd.

 MKURUGENZI wa SOS Zanzibar, Suleiman Mahmoud Jabir akitowa maelezo ya watoto wanaoishi katika Kijiji hicho kwa Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipofika kuwatembelea.

 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akimpa mkono wa Idd mmoja wa mtoto anayeishi katika kijiji hicho cha watoto yatima cha SOS Mombasa Zanzibar,



 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,Wake wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Pili Balozi Seif na Mama Asha Balozi Seif, wakitowa mkono wa Idd El Fitri kwa watoto wa Kijiji cha SOS Mombasa Zanzibar.   
 WATOTO wa Kijiji SOS Zanzibar  wakimlaki Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein alipofika Kijijini hapo.

 MKE wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwasalimia Watoto wa Nyumba ya Mayatima Mazizini, alipofika kuwapa mkono wa Idd.


Sikukuu yangu! Ndivyo inavyoonekana kwa mtoto ambaye alikuwa akipokea sikukuu yake kutoka kwa Mke wa Rais wa Zanzibar

 MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akitowa mkono wa Idd kwa watoto wa nyumba ya watoto yatima Mazizini.

WATOTO wa Nyumba ya watoto yatima Mazizini wakiwa na bahasha zao za zawadi waliopewa na Mke wa Rais wa Zanzibar alipofika kuwapa mkono wa Idd El Fitri katika makazi yao Mazizini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.