Na Zuhura Msabah, Pemba
RAIS wa Comoro, Omar Ali Msham (22) na Mohammed Said Mbwana wamenusurika kufa maji baada ya kuokotwa pembeni ya ufukwe wa bahari ya kisiwa cha Kojani.
Wacomoro hao waliokotwa na wananchi wa kisiwa cha Kojani ambapo hali zao hazikuza nzuri sana wakati walipokuwata ufukweni mwa bahari hiyo.
Aidha taarifa zinaeleza kuwa walipohojiwa raia hao wa Comoro walijieleza kuwa wao ni wavuvi wanaotokea katika kijiji cha Hansinzi na walipotea baharini tangu Agosti 1 mwaka huu.
Walieleza kuwa wamepotea baada ya mashua yao ya uvuvi kupigwa na dhoruba wakiwa kwenye harakati zao za uvuvi ambapo upepo ulisababisha chombo hicho kupanda mwamba na mashine kutumbukia baharini.
Dakatari wa zamu katika hospitali ya Wete ambako majeruhi hao wamelazwa alisema kuwa hali zao zinaendelea vizuri na walikuwa wamepoteza nguvu kutokana na njaa ya muda mrefu na machofu waliyoyapata.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba, SACP Yahya Rashid Bugi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa ripoti zimeshapigwa katika ofisi ya Idara ya Uhamiaji.
Alisema mara baada ya majeruhi hao kutengemaa kwa afya zao sheria za uhamiaji zitafuata.
Kamanda huyo alitoa wito kwa wavuvi katika mkoa huo kuwa makini kwenye shughuli zao za uvuvi kutokana na upepo unaoendelea ambapo tahadhari isipochukuliwa unaweza kuleta athari.
No comments:
Post a Comment