

Mtaalamu wa Kampuni ya Green Field kutoka Uholanzi, John Krimpex akimuonesha ubora wa nyasi bandia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati alipofanya ziara ya ghafla Uwanja wa Gombani, Chake Chake Kisiwani Pemba
Harakati za uwekaji wa Nyasi bandia katika Kiwanja cha Michezo cha Gombani Kisiwani Pemba zimeanza katika hatua nzuri ya kuridhisha.
Uwekaji huo wa Nyasi unafanywa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Ufundi ya Green Field kutoka Nchini Holland.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amefanya ziara fupi ya ghafla kuangalia maendeleo ya uwekaji huo wa Nyasi Bandia.
Mtaalam wa Kampuni hiyo ya Green Field John Krimen alimueleza Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwamba uwekaji wa nyasi hizo unatarajiwa kukamilika rasmi mwishoni mwa mwezi huu.
John Krimen amesema hatua ya awali ya utandikaji huo unaendelea kama program ilivyopangwa ambao utachukuwa kwa karibu wiki tatu kuanzia Alhamis ya wiki hii.
Alisema mbali ya matumizi ya mchezo wa soka katika Kiwanja hicho lakini pia nyasi hizo zinauwezo wa kuhudumia michezo mengine kama vile gwaride na Hlaiki na uingizaji wa magari ndani ya eneo la kati la uwanja huo ni kuhatarisha umadhubuti wa nyasi hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesifu juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Wataalamu hao za kukamilisha kazi hiyo kwa wakati.
Balozi Seif amesema hatuPublish Posta hiyo itatoa fursa kwa wanamichezo kutumia kiwanja hicho katika mazingira ya kisasa zaidi.
Uwekaji wa nyasi Bandia katika kiwanja cha Michezo cha Gombani Pemba ambazo zina uwezo wa kutumika katika kipindi cha karibu miaka kumi unasimamiwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa FIFA kwa ushirikiano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Othaman Khamis Ame
Ofisi ya Makamau wa Pili wa Rais wa Zanzibar
No comments:
Post a Comment