Habari za Punde

DK SHEIN YUPO GANDO/BOPWE KUWAFARIJI WANANCHI


Miongoni mwa Wazee waliofiliwa na jamaa,ndugu na watoto wao katika shehia ya Gando wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, aklipofika kuwapa pole kutokana na ajali ya kuzama kwa Meli ya MV Spice Islander,iliyozama hivi karibuni katika mkondo wa Nungwi.


Wananchi wa kijiji cha Bopwe wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba, wakimsikiza Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein,alipofika kuwapa pole ,kwa kufiliwa na jamaa zao waliofariki kwa ajali ya meli Mv Spice islander hivi karibuni,Mazungumzo na wananchi hao yalifanyika katika skuli ya Pobwe Wete Pemba, wilaya ya Wete,Pemba

Wananchi wa kijiji cha Gando wakimsikiza Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, alipofika kuwapa pole ,kwa kufiliwa na jamaa zao waliofariki kwa ajali ya meli Mv Spice islander hivi karibuni. Mazungumzo na wananchi hao yalifanyika katika skuli ya sekondari ya Gando Wilaya ya Wete,Pemba.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akiwapungia mkono wananchi wa Gando alipofika katika skuli ya kijiji hicho, alipofanya ziara maalum ya kuwapa pole wafiwa katika ajali ya meli ya Mv Spice Islander,hivi karibuni

Picha zote na Ramadhan Othman, Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.