MKURUGENZI wa Kampuni inayotoa huduma kiwanja cha Ndege cha Zanzibar (ZAT),Tobi Marhun (kushoto), akimkabidhi shilingi milioni kumi Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mama Asha Seif Iddi, kwa ajili ya waathirika wa ajali ya meli ya MV. Spice Islanders wiki ilioyopita. Kulia Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Mohammed Raza.
MWAKILISHI wa Viti maalum na Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi, Mgeni Hassan Juma, akimkabidhi shilingi milioni mbili, Makamu wa Pili wa Rais kwa niaba ya Wabunge wa Jumuia ya Afrika Mashariki kusaidia waathirika wa ajali ya meli iliyotokea wiki iliyopita huko Nungwi.
RAIS wa Shirikisho la Jumuia ya Waislamu wa Khoja Shia Ithna-Asher Afrika Mashariki, Alhajj Anwarali Daramsi, akimkabidhi hundi ya shilingi milioni thelathini, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia maafa ya kuzama kwa meli.
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Pandu Ameir Kificho, akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, msaada wa shilingi milioni 15 kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo kusaidia wathirika wa ajali ya meli iliyotokea Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
AFISA wa kitengo cha Mahusiano Benki ya NMB Shy-Rose Bhanji kulia, akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 20, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kusaidia watu walioathirika katika ajali ya meli iliyotokea wiki iliyopita katika mkondo wa Nungwi. Kushoto Meneja wa NMB tawi la Zanzibar, Mluku Abdallah.
No comments:
Post a Comment